Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka
saini hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti
4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na
Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka
saini hati ya Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia
Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam
akishuhudiwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akigonga
muhuri wake hati ya Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne,
Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa
na Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Mhandisi Ngosi Mwihava.
Rais Kikwete akipeana mikono na
Waziri wa Nishati na Madini Mhe George Simbachawene baada ya kuweka
saini kuridhia Muswada wa Sheria ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne, Agosti
4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka
saini kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia
Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam
akishuhudiwa na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya na Katibu Mkuu wizara
hiyo Dkt. Servacius Likwelile.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana
mikono na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya baada ya kuweka saini
kuridhia Muswada wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia Jumanne,
Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka
saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti 4, 2015 katika
Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam akishuhudiwa na Dkt. Shukuru
Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana
mikono na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa
baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu Jumanne, Agosti
4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam kulia ni Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo Profesa Sifuni Mchome.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana
mikono na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa
Sifuni Mchome baada ya kuweka saini kuridhia Muswada wa Tume ya Walimu
Jumanne, Agosti 4, 2015 katika Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa
Rais Dkt. Mohamed Gharib Bilali, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue katika picha ya pamoja na Mheshimiwa George Simbachawene, Waziri
wa Nishati na Madini, Mheshimiwa Saada Mkuya, Waziri wa Fedha na Mhe.
Dkt. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi baada ya
hafla ya kuweka saini na kuridhia miswada ya Sheria ya Mafuta na
Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada wa Usimamizi wa
Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya Bidhaa na Muswada
wa Tume ya Walimu. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Agosti 4, 2015,
ametia saini Miswada ya Sheria mitano hadharani ikiwa ni hatua yake ya
mwisho kabisa kuridhia Miswada ya Sheria akiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Katika sherehe iliyofanyika katika
Ukumbi mpya wa Ikulu, Dar Es Salaam,Rais Kikwete ameridhia Muswada wa
Sheria ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Uwazi na Uwajibikaji, Muswada
wa Usimamizi wa Mapato ya Mafuta na Gesiasilia, Muswada wa Masoko ya
Bidhaa na Muswada wa Tume ya Walimu.
Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa
na mamia ya wageni waalikwa, mawaziri wanaohusika na sekta hizo,
Mheshimiwa George Simbachawene ambaye ni Waziri wa Nishati na Madini,
Mheshimiwa Saada Mkuya ambaye ni Waziri wa Fedha na Mhe. Dkt. Shukuru
Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wametoa maelezo
ya miswada hiyo mitano kabla haijaridhiwa na Rais Kikwete.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue pia wamehudhuria sherehe hizo ambazo vile
vile zimehudhuriwa na mawaziri wa Serikali, mabalozi, wawakilishi wa
taasisi zisizokuwa za Kiserikali (NGO’s) na wadau wengine wa sekta
ambazo Miswada yake imeridhiwa.
Hiyo ni mara ya pili kwa Rais Kikwete
kuridhia Miswada ya Sheria hadharani. Mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2009
wakati Rais Kikwete aliporidhia hadharani Muswada wa Sheria ya Matumizi
ya Fedha katika Uchaguzi.
Aidha, hiio ni mara ya mwisho kwa
Rais Kikwete kuridhia Miswada ya Sheria nchini kabla ya kuondoka
madarakani mwanzoni mwa Novemba, 2015. Rais tayari amelivunja Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
4 Agosti, 2015













Note: Only a member of this blog may post a comment.