Saturday, August 29, 2015

Anonymous

PICHAZ: SHUHUDIA LOWASSA ALIVYOKUTANA NA WANAFUNZI NA WAJASIRIAMALI JIJINI DAR ES SALAAM

Mgombea urais wa vyama hivyo Mh Edward Lowassa na mgombea mwenza Mh Duni Haji wamekutana na makundi mbalimbali ya wajasiriamali na wanafunzi wa elimu ya juu ambao licha kutumia fursa hiyo kuelezea matatizo yanayowakabili wametoa mapendekezo yatayolenga kuwawezesha watanzania kunufaika na rasilimali za nchi yao.

Wawakilishi wa makundi hayo wamesema hatua ya kuviunganisha vyama vya siasa na kupatikana UKAWA imewapa matumaiani makubwa ya kuondokana na uonevu na umaskini mkubwa unaowakabili.

Akizungumza na makundi hayo Mh Lowassa na viongozi wengine wa UKAWA wamesema wamejipanga ipasavyo kuleta na kusimamia mabadiliko ya kweli yatakayotatua kero za wananchi na kuondoa uonevu uliokidhiri matatizo ambazo serikali ya ccm imeshindwa kuyapatia ufumbuzi kwa miaka yoyte 50 iliyokuwa madarakani.
Msanii Juma Nature A.k.a Kibla akiongoza wasanii wenzake kuwasalimia viongozi wa UKAWA leo Ijumaa 28/08/2015 ikiwa ni majumuisho ya ziara ya Mgombea Urais Mhe. Lowassa kwa jiji la Dar es salaam




Mhe. Edward Ngoyai Lowassa awasili katika viwanja vya Msimbazi Center

Mhe. Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya Msimbazi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuongea na wawakilishi wa vikundi mbalimbali kutoka Dar es salaam leo Ijumaa 28/08/2015

Mhe. Edward Lowassa akiwasili katika viwanja vya Msimbazi jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuongea na wawakilishi wa vikundi mbalimbali kutoka Dar es salaam leo Ijumaa 28/08/2015

M/kiti wa CHADEMA Mhe. Mbowe akiwasili Msimbazi Centre kufanya mjumuisho wa ziara ya mgombea Urais Dar

Meza kuu kwenye mkutano

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.