Staa wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’.
Hamida hassan
Yamemkuta! Staa wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’ ameonja joto ya jiwe baada ya kuwekwa chini ya ulinzi mkali huko Hong Kong, China ambapo alidhaniwa kuwa amebeba madawa ya kulevya ‘unga’.
Yamemkuta! Staa wa Bongo Movies, Salma Jabu ‘Nisha’ ameonja joto ya jiwe baada ya kuwekwa chini ya ulinzi mkali huko Hong Kong, China ambapo alidhaniwa kuwa amebeba madawa ya kulevya ‘unga’.
Akizungumza
na Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Nisha alisema kuwa alijikuta
akiichukia nchi ya China baada ya kupata wakati mgumu alipowekwa chini
ya ulinzi kwa muda wa saa nne.
“Yaani China si mchezo, ukienda uwe na
sababu, bila sababu unaweza kujikuta unaishia jela, kwa sasa Watanzania
hatuaminiki kabisa, mwenzenu nilikamatwa na kupekuliwa mpaka
walipojiridhisha ndipo wakaniachia,” alisema Nisha.

Note: Only a member of this blog may post a comment.