Soudy Brown
huwa anazinasa stori za chinichini, anachokifanya ni kuwatafuta
wahusika na kucheki nao kama kwenye hizo za chinichini zina ukweli au ni
za kuzushwa, iliyomfikia jamaa leo inahusu ishu ya staa wa Muziki Meninah la Diva kuolewa.
Gossip Cop akaamua kumcheki kaka wa Meninah kwa
sababu Meninah mwenyewe yuko honeymoon.. kaka amesema ndoa ilikuwa ya
ghafla na kila kitu walikisimamia wenyewe kama Familia, hakukuwa na
michango yoyote iliyokusanywa ili kufanikisha… ndoa ya Meninah na mtoto na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo imefanyika Jumapili nyumbani kwa akina Meninah, Kigamboni Dar.
Muziki je anauachaje? Kaka wa Meninah
amesema japo dada yake kaolewa lakini ataendelea kufanya muziki lakini
kutakuwa na mabadiliko kidogo tu kwenye aina ya muziki atakaoufanya.
U Heard iko kwenye hii sauti pia mdau wangu.
Note: Only a member of this blog may post a comment.