Mwanzoni mwa mwezi July kulikuwa na habari mbalimbali zilizoweka headlines katika mitandao ya kijamii kuhusu mchezaji wa Yanga Simon Msuva na baba yake Mzee Msuva, kila mtu alikuwa anazungumza kuhusiana na Simon Msuva.
August 3 Simon Msuva aliongea na millardayo.com na kuweka wazi kuhusiana na taarifa za yeye kupuuza ushauri wa baba yake, awali kulikuwa na uvumi kuwa baba yake Simon Msuva alimshauri aondoke Yanga na kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine hususani klabu ya Simba ambayo baba yake ndio klabu anayoipenda.
Msuva amezungumzia hizo taarifa za baba yake kutaka aondoke Yanga
“kiukweli
Mzee anamapungufu yake siwezi kumuongelea sana sababu yeye sio mtu
anayeniongelea mimi, mtu anayeniongelea mimi ni Management yangu ambayo
inaweza ikaongea kila kitu kuhusu mimi”>>> Simon Msuva
“kwa hiyo mzee anaweza ongea chochote
kama mzazi, mzee kama mzee anaweza akawa kaongea ila watu wakamuelewa
vingine. Mzee hawezi kuongea sitaki mwanangu acheze Yanga aende nje au
acheze Simba hicho kitu nakataa inawezekana waandishi labda wakawa
wamemuuliza hivyo inategemea si unajua waandishi
wanavyouliza “>>>Simon Msuva

Note: Only a member of this blog may post a comment.