Tuesday, August 25, 2015

Anonymous

Mwacheni MINGU aitwe MUNGU!

IMG_0033IMG_0022
Feruzi Suleiman akipoteza mikono yake kutokana na ajali.
Na Haruni Sanchawa
Hujafa hujaumbika, kauli hiyo ya wahenga imedhihirishwa katika matukio mawili ambayo yanafanana lakini ni kwa watu wawili tofauti, mmoja ni Feruzi Suleiman (27) ambaye amekatwa mikono na mwingine nit Lazaro Modes (40) aliyekatwa miguu.
Ajabu ni kwamba wote chanzo chao cha kupoteza viungo hivyo ni umeme.
Wagonjwa hao wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Wodi ya Sewa Haji namba 23, na sababu kuu wanasema ni hitilafu ya umeme. 

ILIKUWAJE KWA FERUZ KUPOTEZA MIGUU?
Feruzi aliyekatwa miguu ambaye ni mkazi wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam anasimulia:
“Mimi ni fundi umeme ambaye nafanya shughuli zangu kwa kujitegemea.
“Julai mosi mwaka huu niliitwa na rafiki yangu Hashim ambaye ni fundi umeme, ili tukafunge umeme kwenye nyumba moja iliyoko Goba, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Niliitikia wito wa rafiki yangu huyo tukaungana kuelekea huko na tukakutana na tajiri yetu ambaye jina lake silifahamu kwa sababu ilikuwa ni mara ya kwanza kumuona lakini nyumba yake ilikuwa ya ghorofa moja.
IMG_0044
Lazaro Modes akipoteza miguu.
Tulipofika tulipewa maelekezo na tajiri huyo tukaanza kupanda ghorofani kwa maana ya kuanza kazi, kumbe kuna baadhi ya nyaya zilikuwa na umeme hivyo kunirusha kutoka ghorofa ya pili hadi chini na kufanya nipoteze fahamu kwa saa nne.
Nilikimbizwa katika Zahanati ya Goba na kulazwa pale kwa muda wa siku mbili kisha kutolewa na kuhamishiwa Hospitali ya Mwananyamala. 

Nilipofikishwa nililazwa lakini kutokana na hitilafu ile iliyonipiga kuanzia ubavu wangu wa kushoto na kuchukua sehemu yote ya kiuno ambayo ilikufa ganzi.
“Hospitali ya Mwananyamala hawakuweza kusaidia lolote kutokana na ugumu wa tatizo hilo kuwa juu ya uwezo wao.“Walipoona hali inazidi kuwa tete walinihamishia Hospitali ya Muhimbili na kulazwa Sewa Haji wodi namba 23.
“Miguu ilianza kuoza na kutoa funza, madaktari wakaamua kuikata.
 
“Jijini Dar es Salaam ninao ndugu wawili wa kuzaliwa lakini ndiyo hawana uwezo wa kusaidia lolote kwa tatizo langu, chakula na dawa napata kutoka kwa wauguzi na wasamaria wema,” alisema huku akitokwa na machozi.Kwa yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasiliana na mgonjwa huyu kwa namba 0654 830584. 

ILIKUWAJE NAYE LAZARO KUPOTEZA MIKONO?
Naye Lazaro Modest ambaye ni mkazi wa Jangwani jijini Dar es Salaama, amekatwa mikono kwa tatizo kama la Feruzi.
IMG_0033Modest anasema: “Ilikuwa Juni 23, mwaka huu nilipokwenda katika duka moja la kununua vifaa vya umeme, na shida yangu ilikuwa ni kupata bomba kwa ajili kutengenezea mlango wa geti.
“Nia yangu ilikuwa kwenda kuimarisha ubora wa geti lililoko nyumbani kwangu.
“Nilinunua bomba lenye urefu wa futi 20, nilienda nalo hadi kwangu, nilipofika karibu na geti nilishtukia nimetupwa mbali.
“Nilisahau kuwa eneo lile kulikuwa na waya wa umeme ulishuka chini.
 
“Ule waya ulikuwa na umeme hivyo kugusana na lile bomba nikapigwa shoti ya umeme, nikatupwa chini na kupoteza fahamu.
“Nilipozinduka nilijikuta nikiwa nipo Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar lakini kutokana hali yangu kuwa mbaya baada ya siku nne nilihamishiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Hali yangu ilikuwa mbaya na wataalamu wakawa hawana jinsi hivyo kulazimika kukata mikono.
 
“Madaktari waliniambia nafuu yangu ni kukatatwa mikono na hivi sasa najiona sina faida, nitafanya kazi gani nikipona?
“Shughuli zangu za kujitegemea zimeyeyuka,” alisema mgonjwa huyo kwa huzuni.
Kwa aliyeguswa na habari hii anaweza kuwasiliana na mgonjwa huyu kwa namba 0762 755181

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.