“Hata sijui nianzie wapi, kuna siku kundi la watu walifika ofisini kwangu, nilipohoji ujio huo kwa kuwa haukuwa wa amani, nikajibiwa kwa kuoneshwa kidole kwa dada mmoja aliyeshukiwa kuchukua mume wa mwenzie. Mara wakaanza kurushiana maneno machafu, nusura wakunjane, nikawazuia na kutaka kujua kulikoni.
“Dada mmoja akaniambia kuwa binti aliyekuwa mbele yetu, anatembea na mumewe kwamba siku hiyo aliichukua namba yake kutoka kwenye simu ya mume wake na kuanza kuchat naye akijifanya ndiye yeye. Alizungumza naye mambo mengi na mwishowe akamtaka aje sehemu wakutane, dada huyo bila kujua kuwa anaingia mtegoni, akaenda.
“Baada ya kufika alipo, akakutana naye, akamuuliza alichokifuata eneo hilo, huyo mwanadada akaanza kujiumauma, akidai kuna mtu anamsubiri, basi akampigia simu yake, akasogea pembeni ili akazungumze, huyo dada mwenye mume akakata simu, akamfuata na kumzaba vibao, akimwambia yeye ndiye aliyempigia na kumuuliza kwa nini anatembea na mume wake.
“Akasema watu waliwakuta wakizozana, wakawashauri kuja ofisini kwangu, wakiwa hapa ndipo yule dada akaanza kuvua nguo ili kati yao aonekane mzuri ni nani ndipo nilimzuia na kumwambia kufanya vile ilikuwa ni kujidhalilisha, yule dada alimuomba msamaha kwamba asingerudia kutoka na mumewe aliyemdanganya.
Kama una kituko kilichowahi kukutokea ukiwa ofisini wasiliana nasi kupitia namba iliyopo hapo juu. Angalizo ni lazima uwe Mwenyekiti, Mtendaji au Mjumbe wa Shina, Kijiji au Mtaa.


Note: Only a member of this blog may post a comment.