Imelda Mtema na Musa Mateja
MSIBA! Staa mwenye umri mdogo
anayekimbiza katika filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amepata pigo
baada ya kufiwa na bibi yake mzaa mama, Leonadina Mboneko (pichani),
aliyefariki dunia juzi asubuhi katika Hospitali ya Masana, iliyopo Mbezi
jijini Dar es Salaam.
“Nimehangaika naye kwa muda mrefu ili
kurejesha afya yake, lakini hali ilikuwa ngumu hadi juzi Mwenyezi Mungu
alipomchukua. Tumepata pigo kubwa sana hasa mwanangu Lulu kwa sababu
alikuwa ndiye kipenzi chake,” alisema mama huyo.
Muigizaji huyo aliyecheza Filamu ya
Foolish Age hakuweza kupatikana kuzungumzia msiba wa kipenzi chake huyo,
lakini nyumbani kwa mama yake, mipango ya kusafirisha mwili huo kwenda
Bukoba, Kagera kwa ajili ya mazishi ilikuwa ikifanyika.

Note: Only a member of this blog may post a comment.