Nahodha wa Dar Es Salaam Young African pamoja na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro amezungumzia kuhusiana na zile taarifa za yeye kuhitajika na klabu ya Al Ahly ya Misri ambazo ziliishia kimya kimya. Cannavaro alihusishwa kujiunga na klabu ya Al Ahly baada ya kuonekana uwezo wake kwenye mechi ya Yanga dhidi ya Al Ahly.
Cannavaro uwezo wake ulionekana katika mchezo wa pili wa marudiano uliochezwa mwanzoni mwa mwaka 2014 Misri ambapo Yanga ilifungwa goli 1-0 nakulazimika kwenda katika hatua ya mikwaju ya penati baada ya ule mchezo wa awali uliopigwa Dar Es Salaam kumalizika kwa Yanga kushinda goli 1-0.
Cannavaro
kama mmoja wa watu walioonyesha uwezo mzuri katika dakika zote 90 na
hata katika hatua ya mikwaju ya penati uwezo wake uliwavutia viongozi wa
Al Ahly ya Misri kiasi kwamba walienda hadi hotel waliofikia Yanga na kuongea na kiongozi wa Yanga.
“Ilikuwa ni kweli ila uongozi wetu sisi na Al Ahly
kidogo ulikuwa sio mzuri kutokana na yule kocha alitufuata hotelini na
aliongea na Vice president wetu na baada ya hapo mazungumzo yalikuwa
yameenda vizuri ila yule kocha alifukuzwa Al Ahly ndio maana ikawa
kidogo imekatika ila tu maendeleo yalikuwa mazuri sana kutokana kwamba
Yanga walikuwa wanahitaji milioni 200 kama sikosei”>>> Cannavaro
Nikukumbushe tu mdau wangu ilivyokuwa katika mchezo na penati ya Cannavaro katika video hiyo hao chini!

Note: Only a member of this blog may post a comment.