Wednesday, August 5, 2015

Anonymous

Ilivyokuwa safari ya SIMON MSUVA kwenda kufanya majaribio Bidvest Wits ya Afrika Kusini!

Simon Msuva ni winga mshambuliaji wa klabu ya Dar Es Salaam Young African ambae msimu uliomalizika aliibuka kuwa mfungaji wa bora wa Ligi Kuu Tanzania bara katika msimu uliomalizika wa mwaka 2014/2015. Awali kulikuwa na taarifa za Simon Msuva kwenda kufanya majaribio pasipo ridhaa ya viongozi wa Yanga.

MSUVA2

Msuva alipata nafasi ya kuongea na timu ya millardayo.com na kuelezea namna ya safari yake ya kwenda Afrika ya Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Bidvest Wits FC ilivyokuwa.

“In short ilikuwa hivi ile timu ilileta ofa lakini ile ofa waliileta katika mazingira ambayo Yanga hawakuwa wamerizika waliona  kama imeletwa kihuni, nazungumzia kihuni kwa sababu haikufika kwa Uongozi moja kwa moja ilikuja ila ikawa imefahamika kuwa Simon anatakiwa kwenda katika timu akafanye majaribio  ili yule kocha aweze kumchukua katika timu nikaletewa tiketi”

Simon Msuva akiwa Afrika Kusini kwa ajili ya majaribio
“Kabla sijaondoka siku mbili mbele nikawaambia viongozi, wakaniambia kwamba Simon huwezi kuondoka bado kuna mechi mbili ya Azam FC na Ndanda, ila nikawaambia ubingwa tushatangaza ila wakagoma na mimi unahitajika South kabla ya Ligi haijaisha ila kocha akanikubali baadae dau walilokuwa wanataka Yanga na wale wakawa wameshindwana”

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.