Friday, August 14, 2015

Anonymous

MBATIA Ashusha Kombora CCM...Afunguka UKAWA Kutotishwa!

James-Mbatia
Na Neophitius Kyaruzi
MWENYEKITI Mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia (pichani) amesema kuwa Mgombea urais kupitia umoja huo, waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa ana uhakika wa kuingia ikulu na kwamba hababaishwi na ahadi zinazotolewa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi aliliambia gazeti hili hivi karibuni kuwa Ukawa wamejipanga vyema kuhakikisha kuwa mgombea wao anachukua dola na kuongeza kuwa muda wa kampeni utakapowadia wanayo mambo mengi ya kuwaambia wananchi kupitia ilani yao ya uchaguzi ambayo kila Matanzania anayelitakia mema taifa letu ataungana nao.

“Hizi ahadi zinazotolewa na mgombea wa CCM, hazitutishi kwani kampeni zitakapoanza tunayo mambo mazuri ya kuwaeleza Watanzania ambayo yatawapa matumaini katika maisha yao, hivyo muda huo ukifika nina hakika tutaungwa mkono kwa kiasi kikubwa,” alisema Mbatia.

Aliongeza kuwa, sera namba moja ya Ukawa ni ‘Mama Tanzania kwanza vyama baadaye’ hivyo waliamua kuungana ili kulikomboa taifa na katika hilo wapo makini kuhakikisha wanachukua dola.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.