Monday, August 3, 2015

Anonymous

MASKINI Staa Huyu wa Saladini! Yupo Hoi Kitandani!

saladini 
Staa wa Bongo Movies Ashura Rashid ‘Saladini’.
Chande Abdallah
Sorry! Staa wa Bongo Movies kutoka Kanda ya Ziwa ambaye aliwahi kutamba na Sinema ya Saladini, Ashura Rashid ‘Saladini’ amelazwa katika Hospitali ya Bugando, Mwanza akisumbuliwa na vidonda vya tumbo.

Akizungumza na Ijumaa Wikienda kwa njia ya simu, mume wa Saladini, Jully Tax alisema kuwa mkewe ambaye ni mchungaji alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa zaidi ya miaka 10 ambapo alipata nafuu na kuendelea na shughuli zake kama kawaida.

Jully Tax alisema kuwa hivi karibuni Saladini alirudi nyumbani kwake akitokea kanisani na kuanza kutapika damu hali iliyowashangaza ndugu zake ambao walimpeleka hospitalini ambapo matokeo yalionesha kuwa ameathiriwa na vidonda hivyo. Alikuwa kanisani akimwombea mtu mwenye mapepo lakini ghafla yule mtu alimpiga tumboni ndipo akatibua mambo lakini ameanza kupata huduma hospitali,” alisema Jully Tax.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.