ALIYEKUWA
mke wa muandaaji mahiri wa filamu Bongo George Tyson, ambaye kwa sasa
amejikita kwenye ulimwengu wa filamu, Beatrice Shayo amesema kuwa,
anajuta kuingia kwenye tasnia hiyo kutokana na kutawaliwa na imani za
kishirikina.
Akipiga stori na Amani, Beatrice alisema
awali alikuwa akiyasikia tu hayo mambo pasipo kujua undani wake, baada
ya kujikita kwenye tasnia hiyo ndipo akakumbana na mambo mazito tofauti
na jinsi alivyojiweka kwa kupenda maombi muda wote, sababu alishangazwa
na kitendo cha wasanii wenziye kumlazimisha kufanya ndumba.
“Sanaa yetu imetawaliwa na mambo ya ajabu sikuwahi kuwaza kama hivi
vitu vipo jamani, mbali na rushwa ya ngono hayo ya kurogana ndiyo
usiulize, kuna watu wanaenda kwa waganga kuwashusha nyota wenzao,
isitoshe kuna wakati nilikuwa naenda kambini kucheza movie ambayo
nilipewa dili na msanii mkubwa tu, sasa wenzangu ambao wengine ni mastaa
kabisa (aligoma kuwataja majina) wakaanza kunilazimisha kwamba ili
niwini katika sanaa ni lazima nifanye mambo ya ushirikina vitu ambavyo
sipendi hata kuvisikia nikajikuta nakosa raha,” alisema.

Note: Only a member of this blog may post a comment.