Monday, February 23, 2015

Anonymous

UTATA MTUPU: Gardner Akanusha Uvumi wa Kuachana Mkewe Jack!

Gardner Dibibi ambae ni mume wa mwigizaji wa filamu  Jacqueline Pentezel ‘Jack Chuz’ amekanusha taarifa  zilizoenea mtandao na kwenye magazeti ya udaku kuwa ameachana mke wake Jack. 

Gardner ameimbia Bongomovies.com kuwa taarifa za yeye kuacha na mkwe wake sio za kweli japo kuwa ni kweli walikuwa natofauti za kawaida na wameshazimaliza na pia amekanusha kuwa hakumpa talaka kama ilivyoripotiwa .
“Taarifa hizo sio za kweli, sisi  tuko pamoja, tulikua na matatizo ya kawaida tu lakini hatujaachana na wala sijawai mpa talaka. Gadner alieleza. 

Taarifa hizo zilidai kuwa wawili hawa ambao wamedumu kwenye ndoa kwa miaka miwili na nusu sasa wameachana baada ya Gardner kumpa talaka Jack huku chanzo kikitajwa kuwa ni usaliti katika mapenzi.
JIUNGE NASI FACEBOOK > >>BONYEZA HAPA.KAMA KUNA TATIZO AU UNA PICHA ZA MATUKIO TUTUMIE WHATSAPP +255 712 919 142. 
ASANTE NA KARIBU TENA!

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.