Golikipa mkongwe katika soka la Tanzania ambaye ana historia ya kucheza vilabu kadhaa Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania Ivo Mapunda amekuwa
na tabia ya kuingia uwanjani na taulo jeupe ambalo tumewahi kuliona
mara kadhaa likileta hali ya sinto fahamu kwa wachezaji wa timu pinzani
na hata muamuzi wakati mwingine.
Ivo
amekuwa na utamaduni ambao kwetu ni mgeni kidogo kwani tumezoea kuona
makipa wa Ulaya pekee ndio watu ambao huwa wanaingia na taulo uwanjani
kwa ajili ya kujifutia jasho, ugeni wa kitendo hicho kimekuwa kikileta
utata kwa wachezaji timu pinzani wakiamini kwani hawafungi goli kutokana
na uwepo wa taulo la Ivo nyavuni.
Team ya millardayo
ilipata nafasi ya kufanya exclusive interview na kipa huyo ambaye
utamaduni wa kutumia taulo jeupe wakati wa mechi amekuja nao wakati
akitokea Kenya, ni kwa nini Ivo anatumia taulo jeupe? linaongeza chochote kuweza kumsaidia asifungwe.
“Taulo
halihusiani hata kidogo na mimi kuweza kucheza vizuri au kucheza vibaya
uwanjani, taulo ni kitu ambacho magolikipa ulaya hutumia wakati
wanapojifuta jasho au mvua kunyesha, ila kwa hapa wamekuwa na imani
potofu kwa watu hata nilipokuwa Kenya ila mimi baada ya kuona wachezaji
pinzani wanaathirika kisaikolojia ndio maana nalitumia”>>> Ivo Mapunda
Zaidi msikilize hapa

Note: Only a member of this blog may post a comment.