Monday, August 3, 2015

Anonymous

MAGONJWA HATARI KWA WANAWAKE-3



Leo naendelea kuelezea kuhusu magonjwa hatari kwa wanawake, lengo likiwa kukuelimisha kuhusiana na maradhi hayo.

ATHARI YA KUTOTIBIWA MAPEMA MAGONJWA YA NGONO
Magonjwa haya ya ngono yasipotibiwa mapema na kwa usahihi yanaweza kuleta athari zifuatazo kwa mgonjwa.

KWA WANAWAKE
Kwa mwanamke anaweza kupata tatizo la kuziba mirija ya uzazi na kukumbwa na tatizo la mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi au kutozaa kabisa.

Mgonjwa wa kike asipopata tiba pia anaweza kupata maambukizi katika mfuko wa uzazi au kupata magonjwa katika viungo muhimu mwilini au kukumbwa na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu, kansa ya kizazi pia ataweza kupata mabadiliko ya hedhi.

KWA WANAUME
Kwa kuwa magonjwa hayo huwakumba pia wanaume siyo vibaya nao kuwaelezea hapa kwamba nao wasipopata tiba mapema wanaweza kupata maambukizi katika kokwa za mbegu za uzazi (testis) au kuziba mirija inayopitisha mbegu za uzazi (vas deferens) na kumfanya ashindwe kumpa mimba mwanamke.

Lakini pia anaweza kupata matatizo ya kukojoa kwa sababu ya kuziba njia ya mkojo (urethra), kupata magonjwa katika viungo muhimu mwilini kama ubongo, moyo na figo.

Mgonjwa wa magonjwa ya ngono asipotibiwa mapema anaweza kupatwa na magonjwa ya moyo na mishipa ya damu au kansa ya uume vilevile anaweza kukumbwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. TIBA NA USHAURI
Bila shaka tumeona athari za kutopata tiba mapema kwa mtu aliyepata maambukizi ya magonjwa ya ngono lakini zaweza kuepukika kwani yatatibiwa mgonjwa akiwahi hospitali na kupata tiba ya usahihi.
Hakuna sababu ya kusita au kuogopa kwenda hospitali wala kumwonea aibu daktari kwani magonjwa ya ngono yanatibika isipokuwa Ukimwi.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.