Hali ilivyokuwa katika barabara ya Bibi Titi na Morogoro.
Wafuasi wa vyama vinavyounda Ukawa wakiwa kwenye gari kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa ajili ya kumsindikiza Mgombea Urais kupitia Ukawa, Edward Lowassa.
…umati uliofurika.
Harakati za kuelekea kusindikiza mgombea Urais zikiendelea barabara ya Bibi Titi.
Wafuasi wa vyama vyote wakiwa juu ya gari lao kuelekea Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kumsindikiza Lowassa.
Gari la Mhe. Lowassa likisindikizwa
kuelekea Makao makuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Kinondoni mara baada ya kuchukua fomu.
Wananchi barabarani wakimlaki Lowassa kwa kuonesha ishara ya Chadema.
Ulinzi ulivyoimarishwa.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrosia na
Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe alipowasili katika ofisi za Chama Cha
wananchi (CUF) asubuhi ya leo kabla ya msafara kuanza.
James Lembeli akisalimiana na mmoja wa viongozi wanaounda Ukawa.
Kamanda mkuu wa kikosi cha kutuliza Ghasia (FFU) Ukonga akibadilisha neno na askari mwenzake kama inavyoonekana pichani.
Ester Bulaya (aliyeko juu ya gari kulia akiwa kwenye msafara huo.
Taswira ya msafara wa Lowasa.
Awali, mgombea huyo alianzia Makao Makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), Buguruni, Dar es Salaam kisha kuelekea Tume yaTaifa ya Uchaguzi kwa kupitia barabara ya Uhuru, Bibibti Mohamed hadi Makao Makuu ya Tume hiyo.
Baada ya hapo, msafara wake ulipititia Barabara ya Ocean Road kisha Umoja wa Mataifa, Ally Hassan Mwinyi hadi Makao Makuu ya CHADEMA yaliyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Katika msafara huo, umati mkubwa wa wapenzi na wakereketwa wa mgombea huyo walijitokeza kumsindikiza .
Picha habari, Haruni Sanchawa na Denis Mtima

Note: Only a member of this blog may post a comment.