Tuesday, August 4, 2015

Anonymous

LOWASSA: Itakuwa ni BAHATI MBAYA Sana Wananchi Wakichagua Serikali Tatu!

Mh. Edwad Lowassa alipoulizwa kuhusu sababu za mvutano wa kisiasa nchini, alijibu:
"Kuna mchakato wa uundwaji wa katiba mpya, watu wanataka serikali tatu, wengine moja, wengine wanataka zibaki mbili, lakini mimi kwa maoni yangu naona bora zibaki serikali mbili kama ilivyo sasa, kwa sababu serikali tatu, ile ya muungano itamezwa na Serikali za Tanganyika na Zanzibar na huko ni kuvunja muungano. Kuna watu wameoana pande zote mbili sasa muungano ukivunjika hawa tuta wafanyaje? lakini tuwaachie wananchi watoe maoni".

Alipo ulizwa kuwa wanachi wakipendekeza serikali tatu itakuwaje? Alicheka na kujibu: "Hiyo ni bahati mbaya, itakuwa bahati mbaya sana!"
Source: VOA.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.