Wednesday, August 26, 2015

Anonymous

LOWASSA AFUNGUKA KUHUSU MAISHA YAKE KISIASA!


Edward Ngoyai Lowassa
1 hr · Facebook Mentions ·
Leo ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa na kwa namna ya pekee ninamshukuru Mungu kwa kuendelea kunibariki, kunishika mkono na kuniongoza. Maisha yangu ni mfano wa baraka za Mungu. Kuna nyakati nilianguka lakini kwa upendo wake akaninyanyua na mpaka sasa ameendelea kunionyesha baraka zake. Kwa namna ya pekee ninapenda kuishukuru familia yangu na watanzania wenzangu kiujumla kwa upendo na imani yao juu yangu hata pale nilipopitia vipindi vigumu katika maisha yangu. Nina furaha zaidi leo kwa kuwa ninasherehekea siku yangu ya kuzaliwa nikiwa katika kilele cha mapambano ya kusaidia wananchi wenzangu kumaliza tatizo la umaskini. Asanteni sana.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.