Friday, August 21, 2015

Anonymous

KWENYE SUALA HILI NDIPO NAPOMKUBALIGI NEY WA MITEGO!

Msanii wa Bongofleva Nay wa Mitego ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake wa ‘Sina Muda’ amefunguka na kutoa somo kwa wanaume kwa kuwataka kutowapiga wanawake wao pindi wanapowakosea au wanapotofautiana kutokana na mambo mbalimbali katika maisha ya kila siku.

Nay wa Mitego ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kudai na ujanja wake wote pamoja na ukorofi alionao hajawahi kuthubutu kumpiga mwanamke hata amkosee vipi, ndipo hapo alipokumbushia stori ya kumfumania mpenzi wake na mwanaume mwingine lakini aliamua kuachana na yeye kwa roho safi bila kumfanyia jambo lolote baya zaidi ya kubeba kilicho chake na kuondoka zake.

“Ujanja wangu wote, ukorofi, ubabe lakini sijawai kumpiga mwanamke hata siku moja. Hata uwe umenikosea kiasi gani, nishawahi kumfumania mwanamke wangu akiwa na mwanaume ndani na sikumfanya chochote nilichukua kilicho muhimu nikasepa. Kumpiga mwanamke siyo solution akikushinda mwanamke mwambie wasalimie nyumbani, unatafuta mkali kuliko yeye sababu wapo wengi,” alisema Nay wa Mitego.

Nay wa Mitego alishawahi kuimba wimbo maalum ambao alikuwa akihamasisha wanaume kutowapiga wanawake katika maisha ya kawaida lakini pia msanii huyo anasema anachukia sana na hapendi kuona mwanamke akinyanyaswa kwa kupigwa hata kama kweli atakuwa wamefanya kosa, kwa kuwa anaamini makosa yanaweza kusahihishwa kwa njia mbalimbali tofauti na kipigo.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.