Friday, August 14, 2015

Anonymous

KUMEKUCHA! WASANII WAANDAA TAMASHA KUBWA LA KUHAMASISHA KUPIGA KURA!


Joseph Haule `Profesor J’ akizungumza na waandishi wa habari, wa kwanza kushoto ni mwanamuziki Kala Jeremiah akifuatiwa na Juma Kassim `Juma Nature’.
Msanii wa muziki Bongo, Kala Jeremiah (katikati) akizungumzia tamasha hilo. Kulia kwake ni msanii Joseph Haule `Profesor Jay’ na kushoto ni Juma Kassim ‘Juma Nature’.Msanii `Juma Nature’ akizungumza kwa kina kuhusiana na tamasha hilo, kulia ni Kala Jeremiah na Joseph Haule `Profesor J’ na Msaga sumu. Waandishi wa habari wakifuatilia mazungumzo ya tamasha hilo. Wasanii walioandaa onesho hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja ambapo wa kwanza kushoto ni Kiboya akifuatiwa na Kala Jeremiah, Joseph Haule ‘ Profesor Jay’, Msaga Sumu na Juma Kassim ‘Juma Nature’.
WASANII wa muziki Bongo, Joseph Haule ‘Profesor Jay`, Juma Kassim `Juma Nature’, Kala Jeremiah na Msaga Sumu wameamua kuandaa tamasha maalumu la kuwahamasisha wananchi kupiga kura ambalo wamelipa jina la ‘Democracy in Dar’ ambalo litakalofanyika Agosti 16 kwenye viwanja vya Mbagala Zakhem.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kuhusiana na tamasha hilo litakalopambwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii hao wakiwemo pia Emmanuel Elibarick `Nay wa Mitego’, Emmanuel Mbasha, Roma na wasanii wa Bongo Movie, Jaqueline Wolper, Aunt Ezekiel na wengine wengi, wamesema burudani hiyo haitakuwa na kiingilio ambayo itaanza saa7 mchana hadi saa12 jioni.

“Madhumuni ya tamasha hili ni kutaka kuwakumbusha wananchi na kuwaelekeza umuhimu wa kupiga kura kwa kuwa ni haki ya kila mmoja. Hivyo watu waje kwa wingi ili wapate kutambua umuhimu huo kwani burudani itakuwa haina kiingilio,” alisema Profesor J.
(NA MAYASA MARIWATA/GPL)

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.