Tuesday, August 11, 2015

Anonymous

KINACHOENDELEA KESI YA MCHUNGAJI GWAJIMA HIKI HAPA

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, jana alikiri mahakamani kwamba alishindwa kuhifadhi bastola yake mahali salama, hali iliyosababisha washtakiwa wenzake kukutwa nayo. 

Mbali na Gwajima washtakiwa wengine ni  Askafu Msaidizi wa kanisa hilo, George Mzava; mfanyabiashara, Yekonia Bihagaze  na Mchungaji Georgey Milulu ambao  wanakabiliwa na mashitaka ya kukutwa na bastola bila kibali. 

Gwajima alikiri mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akisomewa maelezo ya awali na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Joseph Maugo katikam Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. 

Pia, alikiri kwamba Machi 23, mwaka huu alilazwa na kuwa chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi, katika hospitali ya TMJ.
Hata hivyo, askofu msaidizi na wenzake walikanusha kufanya jaribio la kumtorosha askofu Gwajima akiwa chini ya ulinzi wa polisi katika hospitali hiyo pamoja na kukutwa na begi lililokuwa na bastola, risasi tatu za bastola na risari 17 za bunduki aina ya Shortgun.
Kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa ushahidi wa Jamhuri Septemba 10, mwaka huu.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.