Keisha ni mmoja wa wasanii walioshindwa kupitia kwenye
kura za kuwapata wabunge wa viti maalum kupitia CCM lakini amesema
hajakata tamaa.
“Zile za kwanza zilikuwa ni kura za maoni nilishinda, then kulikuwa
na kura za kitaifa ambapo nilikuwa mtu wa 4 katika watu 18,” alisema.
“Watu wanaotakiwa ni wawili, kwahiyo wawili ndio walioshinda katika upande wa walemavu. Basi maisha yanaendelea na tunaendelea na kampeni kwa sababu ni chama changu. Lakini hii hatua niliyofikia imenijenga kwa sababu wakati nashiriki, sikutengemea ushindi peke yake, nilijua pia kuna kushindwa kwa sababu kuna watu walianza hiyo safari muda mrefu. Kama hao walioshinda wawili walianzia mwaka 2010, kwahiyo mtu asiyekubali kushindwa siyo mshindani.”
Bongo5

Note: Only a member of this blog may post a comment.