Mchana wa August 13 2015 taarifa zinatoka kwamba Msafara wa mgombea Urais wa Tanzania 2015 kupitia UKAWA Edward Lowassa umezuiwa na Polisi kwenda kwenye mazishi ya mzee Kisumo huko Mwanga Kilimanjaro ambapo baada ya kuzuiwa waligeuza kurudi walikotoka.
Yafuatayo ni mambo sita
ambayo yametoka kwenye kauli ya Polisi Kilimanjaro kupitia kwa kamanda
wake Felgensi Ngonyani mbele ya Waandishi wa habari leo August 14 2015.
1.
Tarehe 13 August 2015 Usangi wilaya ya Mwanga, katika mazishi yale
kulikua na taarifa mbalimbali kwamba viongozi mbaimbali wangehudhuria
akiwemo Rais Jakaya Kikwete na baadae tulipata tetesi kwamba na Edward
Lowassa naye angehudhuria.
2. Kweli
siku husika tukapata taarifa za msafara wa Edward Lowassa ulipopita
Mwanga mjini, nikapata taarifa kutoka kwa mkuu wa Upelelezi Mwanga
kwamba msafara wa Lowassa ukiwa na magari zaidi ya 70 na pikipiki zaidi
600 wanataka kuja kwenye msiba, mimi nilikua kwenye msiba na nikaona
wingi huo wa magari na pikipiki kusingepatikana sehemu ya maegesho.
3. Baada
ya hapo nikawapigia simu Mh. Ndesamburo na James Mbatia ambao nao
walidai wamezuiliwa wasiende kwenye mazishi Usangi, nikaongea nao
nikawambia hali halisi ya huku nikaona ni busara magari ya viongozi
yaani kina Mbatia, wasaidizi wao na walinzi waruhusiwe lakini sio
msafara wa magari mengine na pikipiki.
4.Baada
ya kuwapa taarifa hiyo wale viongozi walikataa kwa kusema hawawezi
kwenda peke yao bia Wafuasi wao, wakaamua warudi walikotoka.
5. Baadae
kukawa na taarifa kwenye mitandao kwamba nimeongea na Waandishi kwamba
kuzuiwa kwa msafara ule kulitokana na shinikizo la viongozi wa ngazi ya
juu na kwamba Polisi tunaonewa ile sio matashi yetu, hiyo ni uzushi na
sikuongea jana na Waandishi wahabari.
6. Baada
ya msafara kuzuiwa kwenda msibani wakaondoka Mwanga na walipofika njia
panda ya Himo wakaweka kituo kwa nia ya kutaka kufanya mkutano wa
hadhara wakapaki barabarani na kuziba njia kila kona, Polisi ilibidi
wapige bomu ili kutawanya ule umati ili watu waweze kupita na kuendelea
na shughuli za kawaida.
Note: Only a member of this blog may post a comment.