Na Richard Manyota
USHAWISHI mkubwa umefanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhakikisha
kuwa, katibu mkuu aliye mapumzikoni wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema), Dk. Wallboard Slaa anashiriki kwenye kampeni ya chama hicho
tawala, Uwazi Mizengwe limeambiwa.
Dk. Wallboard Slaa.
Chanzo kutoka ndani ya CCM kilisema hivi karibuni kuwa, mazungumzo
yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa na kwamba upo uwezekano wa asilimia 90
kwa Dk. Slaa kupanda jukwaani siku ya ufunguzi wa kampeni za CCM
uliopangwa kufanyika kwenye Viwanja vya Jangwani, Dar keshokutwa
Jumapili.
“Ili kukabili nguvu ya upinzani tulipanga kuwa Dokta atoke mafichoni
ashiriki nasi kwenye uzinduzi, tuna imani hilo litafanikiwa na utakuwa
ni mtaji mkubwa kwa chama chetu kipindi hiki cha kuelekea kwenye
uchaguzi mkuu,” kilisema chanzo chetu.
DK. SLAA AMEKUBALI?
Kwa mujibu wa chanzo hicho, pamoja na kutamka wazi kuwa mazungumzo yamefanikiwa kwa kiwango kikubwa lakini suala la ushiriki wa kiongozi huyo kutoka chama cha upinzani kwenye uzinduzi wa kampeni za chama tawala lilikuwa halijaafikiwa na Dk. Slaa kwa asilimia mia moja.

Mgombea urais kupitia CCM, Dk. John Magufuli.
“Bado kuna mambo madogomadogo yanakwamisha lakini wakubwa (chanzo
hakitaji kwa majina wakubwa ni akina nani lakini kwa tafsiri huenda ni
viongozi wa CCM ngazi ya taifa) wamepanga kukutana naye na kufikia
makubaliano.”
Aidha, Mwandishi Wetu alipodadisi mambo hayo madogomadogo ni yepi,
chanzo hicho hakikuweka wazi lakini uwepo wa maafikiano ya hatima ya
kisiasa ya Dk. Slaa lilikuwa jambo la wazi.
KWA NINI DK. SLAA AIPIGIE KAMPENI CCM?
Chanzo ndani ya CCM ambacho kimo kwenye timu ya ushindi ya chama hicho iliyotangazwa hivi karibuni kilisema: “Hakuna kitu kingine zaidi ya kummaliza mpinzani wetu (Edward Lowassa ambaye ni mgombea kutoka vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi kwa kufupi Ukawa.)

“Kwenye uzinduzi tumepanga dokta apande jukwaa moja na mgombea wetu
(John Pombe Magufuli)wafanye mashambulizi, tumalize kazi na tusubiri
kuapishwa. Unadhani wapinzani watakuwa na nguvu tena baada ya hapo?
Hakuna,” chanzo kilimaliza kwa kicheko.
Mazungumzo kati ya mwanasiasa huyo machachari na CCM si habari mpya
kwani imekwisharipotiwa mara kadhaa na vyombo mbalimbali vya habarri
bila kukanushwa na Dk. Slaa ambaye toka amejiondoa ndani ya Chadema
amekuwa hataki kuzungumzia waziwazi hatima yake kisiasa.
Mgombea urais wa Ukawa kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa.
UKAWA HOFU TUPU
Tangu Dk. Slaa ajiondoe Chadema, mwanasiasa huyo amezua hofu miongoni mwa wafuasi wa Ukawa kwamba kutokuwepo kwake kwenye umoja huo kunaweza kupunguza kura za upinzani na kuifanya CCM ipate ushindi mwingine wa tano baada ya mfumo wa vyama vingi na hivyo kuendelea kushika dola.

“Hapo ni chumba cha habari cha Global? Nasikia Dk. Slaa kajiunga
CCM?” alihoji mdau wetu wa habari na mfuasi wa Chadema kutoka Karatu
mkoani Arusha aliyejitambulisha kwa jina moja la Jofrey ambaye alitaka
kupata uthibitisho juu ya uvumi wa mwanasiasa huyo kuhamia chama tawala.
Hata baada ya kuambiwa kuwa habari hizo hazina uthibitisho wa moja
kwa moja, shabiki huyo wa Ukawa aliongeza: “Laa! Sawa kaka kama
unanificha sawa, ila huku hatuna raha kabisa. Yule mzee akijiunga CCM,
itakuwa shida sana Ukawa kupata ushindi.”
MAJIBU YA CCM
Kwa upande wa CCM, msemaji wake ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alipotafutwa na mwanadhisi wetu hakuweza kupatikana lakini mmoja kati ya viongozi waandamizi wa chama hicho ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa sababu yeye si msemaji alikuwa na hayaa:

“Sina taarifa za Dk. Slaa kujiunga na chama chetu wala sijui kama
atatambulishwa kwenye uzinduzi wa kampeni zetu, lakini kwa sisi ambao
tulikwenda vitani tunasema Silaha ya vita haitupwi.” Hakufafanua kama
Dk. Slaa ndiye silaha ya vita au la!
DK. SLAA ANATAFUTWA
Baada ya uwepo wa habari hiyo, jana gazeti hili lilimtafuta Dk. Slaa lakini kama mazoea ya siku za hivi karibuni kiongozi huyo wa zamani wa Chadema hakuweza kupatika kwa njia ya simu na hata alipofuatwa nyumbani kwake, Mbweni jijini Dar haikuwezekana kukutana naye ili azungumzie madai ya kukikampenia CCM.

Hata hivyo, mmoja kati ya watu wake wa karibu ambaye hakupenda
kutajwa jina lake alikana katakata taarifa hiyo kwa madai kuwa, hizo ni
siasa za kujipatia ushindi kupitia nguvu za mtu mwingine.
“Hivi unadhani dokta ni mtu mwepesi kiasi hicho? Huyu ni mtu wa
misimamo sana. Sema watu wamekuwa wakitumia jina lake kujiongezea
nguvu za kisiasa. Hawezi kupanda jukwaani kuinadi CCM, niamini mimi,”
alisema.
UWAZI LACHUNGUZA ZAIDI
Kufuatia taarifa ya Dk. Slaa kuibukia kwenye kampeni kuzagaa na kudokezwa na gazeti moja la kila wiki hapa nchini, timu ya Uwazi Mizengwe iliingia katika uchunguzi kwa lengo la kuchimba zaidi ukweli wa mambo.

Katika uchunguzi wake, timu hiyo ilibaini kuwepo kwa mazungumzo kati
ya mwanasiasa huyo na CCM na kwamba kinara wa ushawihi huo ni kada
maarufu wa chama ambaye amepata kuwa kiongozi mkuu kwenye nchi hii.
Uwazi liliambiwa na chanzo kingine kuwa, Dk. Slaa alikwisha
kuafikiana na mapendekezo ya CCM tangu mwishoni mwa mwezi uliopita na
kwamba alikuwa akimsubiri mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete
arejee kutoka ziarani (nchini Australia) ili kumalizia ngwe ya mwisho
ya makubaliano.
Hata hivyo, mpaka tunakwenda mitamboni ilikuwa haijafahamika kuwa
baada ya rais kurejea kutoka ziarani alikutanishwa na mwasiasa huyo na
kumalizia mazungumzo au jambo hilo halijafanyika na kuvifanya vikwazo
vidogovidogo vilivyotajwa na chanzo chetu cha awali kutoondolewa.
HALI ILIVYO MITAANI
Uchunguzi unaonesha kuwa hali ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu ni 50 kwa 50 na kwamba hakuna chama chochote chenye uhakika wa asilimia mia moja wa kuibuka na ushindi wa kiti cha urais.

Baadhi ya wachunguzi wa mambo ya kisiasa wanasema CCM ina nafasi
kubwa ya kupata ushindi lakini si wa kishindo huku wengine wakitabiri
uwezekano wa Ukawa kupata ushindi wa kushtukiza utakaotokana na
migawanyiko ya wanasiasa na makada wa chama hicho tawala inayokitikisa
chama mwaka huu.

Note: Only a member of this blog may post a comment.