HUWEZI AMINI! Mgombea Huyu Ubunge-CCM Aahidi MSHAHARA Wake Wote Atawapa Wananchi Wake!
Mgombea Ubunge kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi “CCM” jimbo la Rungwe Mkoani Mbeya Sauli Amon, amesema ikiwa atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi wa Jimbo hilo, mshahara wake wote wa ubunge utaingia kwenye akauti ya elimu ya Wilaya ya Rungwe, ili kusaidia shughuli za maendeleo.
Akizungumza na eddy blog team kwenye ofisi za CCM Wilaya ya Rungwe, mara baada ya kurejesha fomu mgombea huyo amesema ikiwa atachaguliwa, atafanya kazi kwa kuzingatia ilani ya chama cha Mapinduzi, pamoja na vipaumbele vyake ambavyo ni pamoja na kuboresha huduma za afya kwa kusomesha madaktari.
Aidha Mgombea huyu pia amesema ataondoa changamoto ya wana Rungwe ya kuuza ndizi zikiwa changa,na kuwa na mfumo wa uuzaji wa ndizi ghalani.
USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK
TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)
Note: Only a member of this blog may post a comment.