Fredrick Bundala aka Skywalker
Kilichomgusa akaamua kufanya hivyo anasema kwanza ni kwa sababu anampenda Dr. Dre, alafu hii sio mara ya kwanza anafanya kurudia wimbo kama alivyofanya kwa huu wa Dre, akataja na list ya nyimbo za mastaa alizowahi kuzirudia ikiwemo wimbo wa Usher Raymond.
Hemedy PhD kwenye headlines nae, sasahivi ana hit ambayo kaibariki kwa jina la ‘Imebaki Story‘… YES YES, hataki kulaza mambo aisee, anasema mipango yake ni kwamba hits nyingine haziko mbali sana kuachiwa… iko ambayo pia anatarajia kuiachia soon, unaambiwa humo ndani kaitaja list ya warembo wote aliowahi kuwa nao, duh.. Tutaisubiri hii !!
Hemedy PhD, staa wa Muziki na Movie Bongo.
Alikuwa na mpango kuitisha usaili wa wanawake ili ampate hapohapo wa kuoa, umeishaje? Majibu ya Hemedy anakiri kwamba ilikuwa tu ni ujana unamsumbua, amekua mtu mzima sasahivi na hata hawazi kufanya hiyo kitu.
Jamaa wa Pah One wanafunga ukurasa, wamesema wana mpango kufanya collabo na Navyo Kenzo washkaji ambao zamani ilikuwa ni kundi moja kabisa… Nahreel member wa Navy Kenzo anasema hawajawasiliana, ila kazi yake ni producer na kama ikitokea biashara kutoka kwa Pah One kufanya nae kazi hatoikataa !!
Hii ndio Pah One ya kwanza, kabla ya Aika na Nahreel kujitoa na kuanzisha Navy Kenzo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.