Wednesday, August 26, 2015

Anonymous

FREEMASONS Wapya WAIBUKA, Wajibadilisha Utambulisho!

Mpenzi msomaji, wiki iliyopita nilieleza uhusiano mkubwa uliokuwepo kati ya Freemasonry ya kale na masuala ya uchawi waliokuwa wakiujua wenyewe tangu zamani. Mambo hayo yote yameelezwa katika Kitabu cha Nehemia kwenye Torati ya Biblia ya Agano la Kale.
SASA ENDELEA…

Kilipita kipindi kirefu baada ya Torati hadi mwaka 1717, walipoibuka Freemasons wapya ambao walijitokeza tena nchini Uingereza wakiwa wengi na nguvu zaidi. Freemasons wa kipindi hicho walikuwa tayari kujibadilisha utambulisho wao kuwaweka mbali na sifa yao ya zamani.

Hata hivyo, hawakupata hadhi isipokuwa kwa wakuu na watawala wa Uingereza na jina walilojichagulia lilikuwa ni jina litakalojulikana na wengi lakini litakaloeleweka na wachache. Ilibidi kulitafsiri upya jina la Freemasons ambalo linalotokana na Kifaransa yaani Ffrerés Masons likiwa na maana ya Ndugu wa Kimasoni. Waingereza ndiyo waliolibadilisha kuwa Freemasons.

Utambulisho huo mpya kwa wajumbe wenye mamlaka za kuamrisha mambo, uliwawezesha Freemasons kuwa na sifa na heshima.

Mwanachama wa mwanzo wa Kimasoni aliyetajwa kimataifa alikuwa ni Frederick, mtoto wa Mfalme wa Wales. Wengine waliofuata walikuwa ni Phillip, mtoto wa Mfalme wa Duke wa Edinburgh na mwandani wa karibu wa Malkia wa leo wa Uingereza, Elizabeth II ambaye yeye mwenyewe ni mlezi wa zamani wa Wamasoni.

Hata hivyo, nyuma ya milango iliyofungwa, Wamasoni walikuwa huru kujihusisha na maadili na kanuni za siri zilizokabidhiwa kwao na wazee wao. Ndizo zilizokuja kuwa msingi wa kiwango cha uanachama kiitwacho digirii.

Wamasoni hawakujihusisha tu na mfumo wa Uingereza peke yake, mawazo yao yalikuwa mbali ya hapo. Miaka iliyofuata baadaye, wakati ambao dunia na Marekani zilitumbukizwa kwenye vita na mapinduzi zaidi na zaidi, mmoja kumshinda mwenziye.

Hayo ndiyo yalikuwa malengo makuu yaliyokuwa yakiaminika kuwa na athari kwa wenye kuonewa. Lakini ukweli ni kwamba mipango ilibuniwa na watu wachache maalum, waliokuwa na njaa ya uongozi katika kila kitu. Yote hayo yalitokea ndani ya nchi zao walizozikimbia kwa karne zilizopita na ndizo zitakuwa msingi wa kuutawala ulimwengu mzima.

Katika karne ya 18, idadi kubwa ya Wafaransa walikuwa ni maskini wakati koo za kifalme na zile zilizojiweza zikiishi kwa starehe na ubadhirifu mkubwa, kukaibuka tofauti kubwa baina ya matabaka hayo mawili.

Wamasoni walitumia matabaka hayo kushurutisha madaraka juu yao na hivyo kusababisha mgongano mkubwa katika historia ya Ufaransa.

Wamasoni walichukua nafasi hiyo ya hali mbaya nchini Ufaransa iliyojaa ghadhabu na wakatumia hilo kufanikisha malengo yao kwa kupanga vizuri vita vya propaganda. Walivihodhi vyombo vyote vya habari kisawasawa na walivitumia kuyapinga maoni ya walio wengi.

Magazeti yalilazimishwa kutangaza mwisho wa utawala wa kifalme na kuanzisha jamii inayofuata uhuru, usawa na ushurutishwaji.

Mamilioni ya fedha yalitumika kuweka chini ya uangalizi hali ya kisiasa ya Ufaransa. Wanasiasa waliofadhiliwa na Wamasoni walihamasisha dhana ya Kimasoni, siri zilizojikita za Wamasoni zilifunguliwa kwa wajumbe wa jeshi la Ufaransa, maofisa wa juu na makamanda waliendeshwa kwa kutumia mawazo ya Wamasoni. Wamasoni walifanya kila jitihada kuwatawala wanasiasa na majeshi ya Ufaransa chini ya Umasoni.

Ilipofika Julai 14, 1789, kundi la watu lilivamia Jela ya Basteel, Paris kisha kuwaachia huru wafungwa. Alama za upinzani uliojikita dhidi ya watawala wa Ufaransa hapo zilidhihirika kwa watu wengi kujitokeza sehemu tofauti nchini Ufaransa.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.