Jenerali Adolphe Nshimirimana.
ALIYEKUWA Mkuu wa Idara ya Ujasusi nchini Burundi na mtu wa karibu wa
Rais Pierre Nkurunziza, Jenerali Adolphe Nshimirimana ameuawa katika
shambulizi la roketi akiwa kwenye gari lake kaskazini mwa Mji wa
Bujumbura leo.
Imeripotiwa kuwa Jenerali Adolphe ameuawa pamoja na walinzi wake watatu katika shambulio hilo.
Jenerali Adolphe Nshimirimana alikuwa rafiki wa karibu wa rais Pierre
Nkurunziza hata baada ya kuondolewa madarakani kama Mkuu wa Idara ya
Ujasusi mwezi Novemba mwaka jana.
Nshimirimana alituhumiwa kwa kusimamia oparesheni za kukabiliana na
waandamanaji baada ya Rais Nkurunziza kutangaza kwamba atawania muhula
wa tatu mbali na kuhusika pia katika kuzima jaribio la mapinduzi dhidi
ya rais huyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.