elewa ni suala la mtu na mtu, si kitu cha pamoja hata kidogo!
Fundisha uwezavyo usitarajie watu wote wakuelewe katika msingi mmoja.
Naamini hata sakata la Josephat Gwajima ambaye ni Askofu wa Kanisa la
Ufufuo na Uzima, lazima litaeleweka tofautitofauti.
Nakatisha maelezo kwa sababu nafahamu jamii ninayoiandikia makala haya inafahamu Gwajima anatuhumiwa kumkashifu Askofu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Kwa msingi huo sitaki kufafanua hatua za sakata lenyewe kutoka kwenye mahubiri ya Gwajima, kukamatwa kwake, kuugua ghafla na kuhamishiwa kwenye chumba cha uangalizi wa karibu kimatibabu (ICU). Nataka kujua, sote tumemwelewa au tungali kwenye mfumo wa uelewa wa mafungumafungu nilioueleza.
Nikiangalia nguvu iliyotumika kumbana Gwajima naona ni kubwa mno ukilinganisha na hali halisi ya tukio lenyewe. Polisi na vyombo vya usalama vilivyoifanyia kazi tuhuma ya askofu huyo wa kanisa la Ufufuo, wamenihakikishia falsafa yangu kuwa inafanya kazi; WATU WANA UELEWA TOFAUTI!
Naam, sina shaka, polisi waliposikia lile linaloitwa ‘Neno la Mungu’ lenye kashfa, lililohubiriwa na Gwajima walielewa tofauti. Waumini wa Kikatoliki walielewa tofauti. Wananchi kwa makundi yao walimwelewa tofauti na hata waumini wa kanisa la askofu huyo nao ni vilevile, uelewa wao juu ya hotuba ile ulikuwa wa tofauti.
Nasema hivi kwa sababu, nimefanya uchunguzi wa kutosha, sikurupuki kuandika na huwa sina desturi ya kuandika nisichokifahamu kwa kina. Alichokihubiri Gwajima kanisani pamoja na maudhui yake kuwa ya ovyo siyo jambo la kwanza kufanywa na viongozi wa dini, zipo nyumba za ibada zinafanya hivyo uchwao.
Siyo tu viongozi wa dini hutumia nyumba za ibada na mimbari za kutolea Neno kutukana na kukashifu dini za wengine; huwatusi mpaka viongozi wakuu wa nchi. Huhubiri visasi na migawanyiko ya dini huku vipaza sauti vikisafirisha sauti umbali utoshao.
Binafsi sijaona kuwepo kwa ushirikiano wa vyombo vya usalama kama niliouona kwa Gwajima ambapo mbali na kuhojiwa polisi, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, naye anataka kuwa na jalada lake la uchunguzi dhidi ya askofu huyo.
Mimi si muumini wa Gwajima, siyo rafiki yake wala sina maslahi naye; taifa ndiyo kila kitu kwangu, ndiyo maana nimelazimika kutafakari zaidi mahubiri yake na nilichomwelewa ndicho nataka kukizungumzia kwa sababu kina maana kwa nchi yangu katika zama hizi za baadhi ya viongozi wa dini kuwa wapambe wa wanasiasa.
Sikiliza mahubiri yote yanayoitwa ya kumkashifu Pengo, acha kuhemkwa na mbwembwe za Gwajima katika uwasilishaji, fuatilia mtiririko kwa akili ya tatu ukifika kwenye maneno haya “INAWEZEKANA (Pengo) KUNA MTU UNAYEMPIGIA DEBE” utajua kuwa msingi wa kadhia hiyo ni ‘utumwa’ wa kisiasa walionao baadhi ya viongozi wa dini.
Sina shaka wakati Gwajima akimtuhumu mwenzake kuwa kuna mtu anampigia debe (asiyemtaja) naye wakati huohuo alikuwa anampigia debe asiyejulikana. Hapa ndipo penye tatizo, hakuna siri tena kwamba daraja la wanasiasa limekuwa nyumba za ibada na wapiga debe wao ni viongozi wa dini.
Nashauri mapema; serikali ikitaka kujenga msingi wa amani, isitumikie mambo ya dini kabisa. Sote tunajua chanzo cha chokochoko ni Mahakama ya Kadhi kupigiwa debe na viongozi wakubwa wa nchi kwamba iingizwe kwenye katiba.
Wasiotaka jambo hilo litokee, mfano, azimio la maaskofu wanapoona mwenzao anawageuka watamtuhumu kupiga debe hata kama nao ni wapiga debe wa mlango wa nyuma. Ni wenye akili ndiyo watakaomwelewa Gwajima, vinginevyo atasulubiwa na utakaso wa dhambi ya udini hautapatikana.

Note: Only a member of this blog may post a comment.