Musa Mateja
Aah! Rais wa Wasafi Classic Baby
(WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond’, juzikati alijikuta akipigwa butwaa
kufuatia kitendo cha mcheza shoo wake, Moses Iyobo ëMozeí na mzazi
mwenzake, Aunt Ezekiel kuoneshana ‘mahaba nipeleke kuzimu’ hadharani,
Risasi Mchanganyiko lilikuwepo kushuhudia.
Tukio hilo la Diamond kupagawishwa na
mahaba ya wawili hao lilijiri usiku wa kuamkia Agosti 3, mwaka huu ndani
ya Ukumbi wa Hoteli ya Regency iliyopo Mikocheni jijini Dar ambapo
kulikuwa na sherehe ya kuzaliwa ‘bethidei’ ya Iyobo. Lakini kabla ya
kufika kwenye tukio hilo, twende hatua kwa hatua.
MWONEKANO WA DIAMOND UKUMBINI
Akiwa kwenye sherehe hiyo iliyojazwa pia
na mastaa, muda mwingi Diamond alionekana mwenye furaha ya hali ya juu
kufuatia mishemishe za bethidei hiyo iliyoandaliwa na Aunt kama moja ya
kumshtukiza ‘sapraizi’ mpenzi wake huyo.
Habari zinasema mpaka Iyobo anaingia ukumbini hapo alikuwa hafahamu kama kuna sherehe ya kuzaliwa kwake.
Rais wa Wasafi Classic Baby (WCB), Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa kabeba keki.
MUDA WA MSHTUKO
Iyobo alizama ukumbini hapo saa 7 usiku kwa kuitwa na Aunt. Aunt pia ni staa wa sinema za Kibongo.
Baada ya Iyobo kuingia ukumbini alipata
mshtuko kufuatia Diamond na nyota wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi
‘Ray’ kumkaribisha kwa kummwagia maji na vinywaji mbalimbali ambapo
waalikwa wengine nao waliungana kumuogesha huku wakimwimbia ‘hepi
bethidei tu yu.’
DIAMOND AFUNGUA SHAMPENI
Baada ya zoezi la kumkaribisha Iyobo
aliyekuwa amelala zake nyumbani kwa Aunt kumalizika, Diamond alipewa
chupa ya kinywaji aina ya shampeni kwa ajili ya kufungulia sherehe hiyo
ambayo ilianza hapo.
Moses Iyobo akiwa kamkumbatia mpenzi wake Aunt Ezekiel.
DIAMOND ACHEZA HUKU NA KULE
Katika hatua nyingine, waalikwa
walitumbua macho kumwangalia Diamond ambaye muda mwingi alikuwa akicheza
tena kwa vituko mbalimbali.
ABEBA KEKI
Pengine ni kwa sababu ilikuwa bethidei
ya mcheza shoo wake, kwani ulipofika wakati wa kupeleka keki mezani,
Diamond aliibeba yeye hadi eneo husika kwa ajili ya ‘kulishania’.
MAHABA NIPELEKE KUZIMU SASA!
Sasa wakati Aunt na Iyobo wakiwa katika
tukio la kulishana keki kwa mtindo wa mahaba nipeleke kuzimu (mdomo kwa
mdomo), Diamond alionekana kushtuka na kuwatumbulia macho (angalia picha
ukurasa wa mbele).
Diamond aliendelea kuwatumbulia macho
kama anayewachungulia huku akipanua mdomo kwa mshangao ambapo wawili hao
wala kiroho hakikuwadunda kwamba wapo laivu.
KUMBE IYOBO ALIFUNDISHWA
Baada ya kuwashangaa wawili hao kwa
karibia sekunde kadhaa, Diamond aliibuka na kusema kuwa, kulishana keki
wawili hao kwa staili hiyo, ndivyo WCB ilivyomfundisha Iyobo kwamba,
anapokuwa na mpenzi wake huyo sharti amlishe kwa kinywa na si kutumia
uma.
DIAMOND HAWEZI KUFANYA HIVI
Jambo ambalo lilijitokeza kwenye sherehe
hiyo ambapo waalikwa walisema katu, Diamond hawezi kulifanya hivyo
kwenye sherehe nyingine (mbali na jukwaani) ni kitendo chake cha kuimba
zaidi ya nyimbo zake tano ukiwemo Nana unaotamba kwa sasa. Huwa
akialikwa mahali, Diamond huimba wimbo mmoja au mbili tu.
Hata hivyo, Diamond mwenyewe alisema
kuimba nyimbo zote hizo na kuruhusu waalikwa kucheza ni moja ya kuonesha
upendo na hamasa yake kwa Iyobo kwani bila yeye hakuna Diamond wala WCB
kwa jumla.
USIRI WA UMRI KAMA KAWAIDA
Hata hivyo, kama kawaida, mpaka mwisho
wa shughuli hiyo, haikuelezwa wazi kwamba, Iyobo alikuwa akisherehekea
kutimiza miaka mingapi ya kuzaliwa kwake zaidi ya kusemwa; ametimiza
miaka kadhaa!

Note: Only a member of this blog may post a comment.