Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari the Boss Lady’
Musa Mateja
Siku za kujifungua za mwandani
wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan
‘Zari the Boss Lady’ sasa zinahesabika.
Habari kutoka kwa chanzo chetu
ndani ya Wasafi Classic Baby (WCB) kimelieleza gazeti hili kwamba, kwa
sasa mwanadada huyo ‘amechoka’ ambapo anatarajiwa kujifungua mwishoni
mwa mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao.
“Kwa sasa yupo Sauzi (Afrika Kusini) na
hatuna uhakika sana kama ataweza kuhudhuria utoaji wa Tuzo za MTV Music
(Mama) wikiendi ijayo,” kilisema chanzo hicho na kuongeza:
“Diamond mwenyewe amekuwa akimuomba sana Mungu amjalie bibiye ajifungue salama.”
Kwa upande wake Diamond alikiri kwamba ni kweli Zari atajifungua muda wowote kuanzia sasa.
“Ni kweli siku zinahesabika. Kama siyo mwezi huu mwishoni, basi itakuwa mwezi ujao,” alisema Diamond.
Kwa sasa Diamond yupo kwenye presha
kubwa ya kuomba mashabiki wake wampigie kura kwa wingi katika Tuzo za
MTV Music (Mama) baada ya kuteuliwa kuwania Vipengele vya Msanii Bora wa
Kiume Afrika, Mtumbuizaji Bora wa Kiume Afrika na Nyimbo Bora ya
Kushirikiana Afrika.
Note: Only a member of this blog may post a comment.