Mastaa wawili wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel na Wema Sepetu.
URAFIKI wa mashaka! Mastaa
wawili wa filamu Bongo, ambao walikuwa mashosti kwa muda mrefu kabla ya
kidudumtu kuingilia kati hivi karibuni na kusuluhishwa, hivi sasa bifu
kati yao limeanza upya, Risasi Mchanganyiko linakujuza.
Chanzo chetu ambacho hakipepesi macho
kinasema tangu Aunt ajifungue mtoto, Wema hakuwahi kukanyaga nyumbani
kwake kwa ajili ya kumuona, kutoa hongera au hata pole kwa rafiki yake
huyo, isipokuwa wamekuwa wakichati kupitia simu za mikononi, kitu
ambacho si sahihi.
“Yaani Aunt kipindi chote alimvumilia
akijua huenda yuko ‘bize’, lakini kwa kutofika kwenye siku hiyo muhimu,
amemtoa kabisa akilini mwake,” kilisema.
Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili
lilimtafuta kwa njia ya simu Aunt ili kuthibitisha ubuyu huo, lakini
akakubali tu juu ya kutohudhuria kwenye tukio hilo muhimu la mtoto wake,
licha ya kuwa alimpa taarifa.
“Hakuja, lakini siwezi mlaumu sana, labda alikuwa na majukumu mengi, ukizingatia hivi sasa ana mambo ya ubunge,” alisema.
Wema hakuweza kupatikana baada ya simu yake kutopokelewa kwa muda wote alipopigiwa.
Note: Only a member of this blog may post a comment.