Brighton Masalu WASTARA Juma
Issa Abeid amekiri kuzidiwa na hisia za kuwa na mwenza kutokana na
ukweli kwamba damu yake bado changa, hivyo suala la kuolewa halikwepeki
huku akimpa nafasi kubwa msanii mwenzake, Bond Bin Sinan endapo atakidhi
vigezo na masharti.
“Mimi ni mwanamke, nimekamilika tena nakula na ninashiba. Damu bado changa. Nikisema siwezi kuolewa, nitakuwa nadanganya. Nimekaa muda mrefu kwa sababu kila mwanaume anayenihitaji ananitamani tu.
“Bond namuona ni mwelewa. Lakini nimempa sharti la kutonigusa hadi siku ya ndoa. Kama atakidhi na hayo mengine ambayo ni siri yetu, niko tayari kuolewa naye,” alisema Wastara.

Note: Only a member of this blog may post a comment.