Kama ilivyo ada, leo tupo tena barabarani kuwakilisha moja ya vituko vilivyopata kutokea katika ofisi za serikali ya mitaa.
Anasema amekutana na kesi nyingi zikiwemo za kifamilia, lakini iliyomvutia zaidi ilikuwa ni ile ya wanandoa ambapo mume alidai kubambikiwa mmoja kati ya watoto wake watatu, kwani kwa maoni yake alifanana mno kwa sura, umbile na hata kutembea na jirani yake aliyekuwa akimhisi kutembea na mkewe kwa muda mrefu.
“Hawa watu walikuwa na ugomvi wa kifamilia kwa muda mrefu, baada ya kushindwana wakaamua kuja kwangu, baada ya mwanaume kuwa wa kwanza kumwaga mboga.
“Mume alisema mtoto wake wa pili kati ya watatu, alikuwa ni wa mtu mwingine kwa sababu hakufanana naye hata kimatendo kwani alikuwa na vituko vingi tena akifanana kabisa na jirani yao kuanzia kutembea, muonekano hata matendo yake.
“Maneno hayo yalimtibua mzazi mwenzake aliyedai kumshangaa mumewe kwa tuhuma hizo na kuhoji alikuwa na uhakika gani kama na wale watoto wawili walikuwa wake?
Mvutano ukawa ni mkubwa kiasi nikalazimika kuwaomba wazazi wa pande zote mbili waje ofisini tuzungumze kwa pamoja.
Mwenyekiti huyo alisema, baba wa mwanaume alimshauri mtoto wake kuacha kusikiliza maneno ya kijiweni na kuyapeleka nyumbani kauli iliyomfanya mwanaye kuangua kilio na kumuomba msamaha mkewe.
Je, wewe ni Mwenyekiti wa
Serikali ya Mtaa au Afisa Mtendaji na una simulizi nzuri iliyotokea
ukiwa ofisini? Kama jibu ni ndiyo, wasiliana nasi kwa ajili ya kuitoa
hewani ili kuifundisha jamii.
Note: Only a member of this blog may post a comment.