Tuesday, July 21, 2015

Anonymous

TUZO YA MTV YAMPA KIWEWE DIAMOND PLATINUMZ!

BAADA ya kuchukuwa Tuzo ya Mtumbuizaji Bora Afrika mwishoni mwa wiki iliyopita, staa anayetikisa kupitia Ngoma ya Nana, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ameonekana kama kupata kiwewe.

Katika kusheherekea usiku wa tuzo hizo zinazojulikana kama MTV Africa (MAMA), Diamond alitupia picha mbalimbali kwenye mitandao yake ya kijamii na mojawapo ilimuonesha akiwa amelala huku tuzo yake ikiwa pembeni ya kitanda na kufunguka; “Nawashukuru madensa wangu kwani wao ndiyo wamenipika nikapikika hadi leo hii.

Shukrani za kipekee zimfikie mama yangu kipenzi Sandra kwa mafunzo na malezi anayonipa kila siku juu ya dunia,” aliandika Diamond na kufanya mashabiki wengi wamuone kama amepata kiwewe kupata tuzo hiyo huku wengine wakihoji kulikoni mbona hajatoa shukrani kwa baba yake.

Kuonesha kiwewe cha kupata tuzo, Diamond alienda mbali zaidi kwa kuandika; “Shukrani za pekee ziende kwa kipenzi changu, Zari kwa raha na usingizi mwanana anipatiao na kunifanya nizidi kutunga zaidi na kuwa mbunifu.” Katika tuzo aliyochukua Diamond, alikuwa akichuana na wakali wengine kama Big Nuz, Mr. Flavour, Mi Casa pamoja na Toofan.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.