Tuesday, July 21, 2015

Anonymous

YA MUNGU MENGI! MTOTO HUYU AVIMBA SEHEMU ZA SIRI JIJINI DAR

Na Mayasa Mariwata
MAMA mmoja Sophia Baltaz (31), mkazi wa Kunduchi jijini Dar es Salaam, amejikuta akilia baada ya mtoto wake, Jovan Msaku (3) kuzaliwa akiwa mzima lakini akakumbwa na ugonjwa wa kuvimba sehemu za siri.

Akizungumza na gazeti hili mama huyo alisema kadiri siku zinavyozidi kwenda ndivyo maisha ya mtoto wake yanavyokuwa hatarini kwani halali kutokana na maumivu makali anayoyapata.

Aliongeza kuwa mwanaye alianza kuugua akiwa na umri wa mwaka moja na nusu kwa kutoka ‘kijiuvimbe’ kidogo pembeni ya uume wake lakini sasa uvimbe huo umeenea sehemu yote nyeti.

“Nikiwa Biharamulo nilikojifungulia, baada ya kuona hali hiyo nilikwenda katika Hospitali ya Teule, madaktari wakaniambia ana tundu kutoka tumboni kushuka chini lakini kwa kuwa bado mdogo wakanishauri aachwe kwani lingeweza kuziba lenyewe,” alisema.

Aliongeza kuwa, mwaka jana alifika Kunduchi jijini Dar kwa dada yake baada ya kuona uvimbe umezidi na mtoto kulia kila wakati, ikabidi aende Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Alisema alipofika katika hospitali hiyo, madaktari walimwambia tatizo la mwanaye linawezekana kutibika nchini.
Mama huyo alisema, aliambiwa asubiri foleni ya watoto wengine waliowahishwa kabla ya wake ambapo upasuaji huo utafanyika mwakani au atakapofikisha miaka mitano. “Niliamua kwenda Hospitali ya Regency kuonana na daktari bingwa wa matatizo hayo.
“Niliambiwa zinahitajika shilingi milioni mbili kukamilisha matibabu yake ili aweze kufanyiwa upasuaji, nawaomba Watanzania wanichangie ili kuokoa maisha ya mwanangu kwani mume wangu hana uwezo huo,” alisema mama huyo. Aliyeguswa awasiliane na mama yake kwa namba 0652 491 532, kutoa ni moyo- Mhariri.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.