Mussa Mateja
Minong’ono! Tumbo la staa wa Bongo
Fleva, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ limezua maswali kwa wadau kibao kama ni
la kawaida au tayari mwandani wake, Naftal Mlawa ‘Nuh Muziwanda’
ameshampachika ujauzito.
Akiwa kwenye tukio hilo, Shilole alizua maswali baada ya tumbo lake kuonekana limejaa kama mjamzito.
“Dah nipo kitambo sasa lakini sijapata picha kama tumbo la Shilole ni mimba au kashiba tu, maana kwa uzoefu wangu jinsi anavyoonekana atakuwa na mimba,” alisema mmoja wa mashuhuda.
Baada ya kuona hali hiyo, mwanahabari wetu alimfuata Shilole kwa lengo la kumtaka azungumzie ishu hiyo kama ni tumbo tu au ameshanasa ujauzito, ambapo alisema:
“Ni kweli nina mwanaume rijali lakini sijabahatika kupata mimba, nadhani muonekano wa tumbo ni kwa sababu ya nguo niliyovaa ila natamani kupata mtoto,” alisema Shilole.

Note: Only a member of this blog may post a comment.