Nicodemus Jonas na Saphyna Mlawa
SIMBA imeandika barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaka mwongozo wa Ramadhani Singano ‘Messi’ kutangazwa mchezaji huru, lakini Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amesema hatotumia keki wala maji ya Azam.
Hans Poppe ametoa kauli hiyo kupinga kitendo cha Azam FC kumsajili Messi siku chache baada ya kuwa huru.
“Azam wameniudhi sana na kuanzia leo sitatumia keki wala maji yao,” alisema Hans Poppe. Hans Poppe pia alisema wameiandikia barua Kamati ya Utendaji ya TFF kutaka mwongozo wa uamuzi wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji chini ya Mwenyekiti, Richard Sinamtwa kumtangaza mchezaji Messi kuwa mchezaji huru.
Hans Poppe aliliambia Championi Jumamosi kuwa: “Haturidhishwi na utendaji wa kamati hii hivyo tumeamua kuandika barua kwenda Kamati ya Utendaji ya TFF tupewe muongozo juu ya utendaji wake wa kazi kwani imekuwa ikituonea sana.”
Hans Poppe alisema anashangaa kamati hiyo kuacha hoja ya msingi ya muda wa mkataba wa Singano na kutoa hukumu kwa kutumia kipengele cha malipo ya malazi (kodi ya nyumba).
“Hii kamati ilituonea kwa (Kelvin) Yondani na (Mbuyu) Twite sasa wametuonea kwa Messi kwa kutumia kipengele kingine kabisa, hii si haki,” alisema Hans Poppe.
Tayari Messi amejiunga na Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili akilipwa dau la Sh Milioni 50.

Note: Only a member of this blog may post a comment.