Mshambuliaji mpya wa Yanga ,Mzimbabwe Donald Ngoma.
Na Khadija Mngwai Dar es Salaam
Mshambuliaji ambaye alishika nafasi ya pili kwa ufungaji msimu
uliopita, Amissi Tambwe aliifungia timu yake bao la pili dakika tano tu
baadaye na kuwafanya mashabiki wa timu hiyo walipuke kwa furaha.
Hata hivyo, Ngoma alifunga bao lake dakika kumi tu baada ya Malimi
Busungu kutoka na nafasi yake kuchukuliwa na Kpah Sherman, hali ambayo
inaonyesha kuwa kombinesheni yao itakuwa hatari sana msimu ujao.
“Tatizo la timu yangu ni kombinesheni kwa sasa, tunatakiwa kwenda
kwenye michuano ya Kagame tukiwa sawa, lakini naona kama vile bado
wachezaji wangu hawajaelewana vizuri,” alisema Kocha wa Yanga, Hans van
Pluijm.
Kwa upande mwingine, straika a zamani wa Yanga, Mkenya Boniface
Ambani, aliyekuwa uwanjani jana, amempigia saluti Ngoma, akisema ni
bonge la straika ambaye atafanya makubwa Bongo.
“Ana uwezo mkubwa wa kufunga mabao. Nafurahia kasi yake ya kukimbia
na mpira na kumiliki kwa kifua. Aina ya uchezaji wake inaendana na soka
la Tanzania, naamini atafunga mabao mengi tu,” alisema Ambani.
Imeandikwa na: Mohammed Mdose, Wilbert Molandi, Hans Mloli na Sweetbert Lukonge

Note: Only a member of this blog may post a comment.