Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam
SIKU chache baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, kutimkia zake nchini Denmark katika Klabu ya Sonderjyske Fodbold, amemvuta nchini humo nyota wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe.
SIKU chache baada ya aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi, kutimkia zake nchini Denmark katika Klabu ya Sonderjyske Fodbold, amemvuta nchini humo nyota wa Yanga, Mrundi, Amissi Tambwe.
Okwi
amejiunga na Sonderjyske Fodboldn hivi karibuni baada ya uongozi wa
klabu hiyo kuvutiwa na kazi yake ambayo amekuwa akionyesha uwanjani
akiwa na kikosi cha Simba na atakuwa akilipwa kitita cha dola 10,000
(zaidi ya Sh milioni 20) kwa mwezi.
Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Mganda, Emmanuel Okwi.
Kutokana na hali hiyo, Okwi atakuwa ni
mchezaji wa pili kutoka katika Klabu ya Simba kulipwa fedha nyingi nje
ya nchi baada ya Mbwana Samatta wa TP Mazembe ambaye pia anachukua
kitita cha dola 10,000 kwa mwezi.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Tambwe
alisema mafanikio ya Okwi ni jambo ambalo kila mmoja angependa kulipata
na hata yeye kama ikitokea atapata bahati kama hiyo aliyoipata Okwi,
basi yupo tayari kuondoka Yanga na kwenda kucheza soka la kulipwa nchini
humo kwa sababu hakuna mchezaji asiyependa mafanikio.
“Kwanza kabisa napenda kumpongeza Okwi kwa bahati hiyo aliyoipata kwani ni jambo zuri na ninamwombea kwa Mungu afanye vizuri.
“Bahati hiyo aliyoipata Okwi hata kama
ningeipata mimi ni lazima ningeenda kwa sababu kila mchezaji anapenda
mafanikio na siyo kitu kingine na kama itatotea na itakuwa na maslahi
mazuri, nitaongea na viongozi wangu na wakiniruhusu nitaenda kufanya
kazi,” alisema Tambwe.
Kutokana maneno hayo ya Tambwe, kwa namna
moja au nyingine unaweza kusema kuwa Okwi amemvutia nyota huyo kwenda
Denmark kwa ajili ya kucheza soka la kulipwa.

Note: Only a member of this blog may post a comment.