Brighton Masalu
STAA mkongwe kunako filamu Bongo, Amri Athuman ‘Mzee
Majuto’ amefungukia shutuma anazopewa na mashabiki wake kwa kupenda
kuonekana na ‘vibinti’ kuwa wanamshobokea mwenyewe.
Staa mkongwe kunako filamu Bongo, Amri Athuman ‘Mzee Majuto’.
Akichezesha taya na Amani, Mzee Majuto
ambaye kifani ni bingwa wa komedi alisema, kutokana na kazi yake ya
uigizaji imemfanya kuzimikiwa haswa na mabinti.
“Sijawahi kumshobokea binti yoyote ila wenyewe ndiyo huwa wananishobokea kutokana na uigizaji wangu,” alisema Mzee Majuto.
Hivi karibuni, Mzee Majuto alidaiwa kuoa
binti mdogo ambaye ni sawa na mjukuu wake mwenye umri wa miaka 18
akidai kuwa sheria ya dini inamruhusu kufunga ndoa wa wake wanne.

Note: Only a member of this blog may post a comment.