Emeka Ike akiwa na mkewe Emma Ike na mmoja wa watoto wao.
KWA mujibu wa habari kutoka katika mahakama moja ya kijadi mjini Lagos, Emma Ike, ambaye ni mke wa mwigizaji maarufu wa filamu wa Nigeria (Nollywood) Emeka Ike, amefungua kesi ya kutaka talaka kutokana na kipigo cha kila mara kutoka kwa mumewe ambaye wamekuwa naye katika ndoa kwa miaka 13.
Akiongea kwa kifupi na waandishi wa habari jijini Abuja jana, Emeka Ike alikiri kwamba ameachana na mkewe huyo. Hata hivyo alikana kwamba wametalikiana.
"Ninapozungumza nawe hivi sasa, sijapata hati ya talaka. Hakuna kitu kama hicho kilichotokea. Sijapata barua yoyote kutoka kwa mtu yeyote. Mimi ni Mkristo na huwa hatutalikiani,” alisema Ike.
Ndoa ya Emeka Ike ilikwama baada ya mwigizaji huyo kuiacha familia yake na kwenda kuishi jijini Abuja na mwanamke mmoja tajiri.
Emma Ike ndiye anayeitunza familia yake ya watoto wanne jijini Lagos hivi sasa ambapo mashabiki wao wanatumaini mgogoro kati ya wawili hao utakwisha kwa ajili ya kuwaokoa watoto wao.

Note: Only a member of this blog may post a comment.