Wednesday, July 8, 2015

Anonymous

MRITHI Wa ANNA MAKINDA Akuta Nyoka Kwenye Gari Yake

Mgombea Ubunge Jimbo la Njombe Kusini, Rose Mayemba ambaye anagombea Jimbo ambalo lilikuwa la Spika Anne Makinda(Pichani juu) juzi alimkuta nyoka amejiviringisha kwenye siti ya abiria kwenye gari yake wakati akiwa Hotelini Njombe. 

Nyoka huyo alikutwa kwenye siti kama abiria anayesubiri dereva aingie awashe gari waondoke, Mbunge huyo alikuwa kwenye Hoteli ambayo walikutana na Viongozi wa CHADEMA. 

Mayemba ambaye ni Mtunza Takwimu Mkuu wa CHADEMA Wilaya ya Njombe alisema baada ya kuingia kwenye gari yake aina ya RAV 4 alishangaa kuona kitu kimejiviringisha kwenye siti ya mbele.

“Nilipokiona hicho kitu wazo la haraka nikajua ni mkanda wa abiria ambaye nilikuwa nimembeba ameusahau… nilipoona ni nyoka anataka kujiviringisha mkononi nilitoka mbio kwenda kuwaita wenzangu” >>> Rose Mayemba. 

Mgombea Ubunge huyo amesema hajui nyoka aliingiaje kwenye gari lake na hawezi kumlaumu mtu ila safari yake Bungeni anamtegemea zaidi MUNGU na hatishiki na chochote.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.