Wakati Ramadhani Gembe anafanya
mtihani wa Taifa wa kidato cha sita miezi miwili iliyopita, hakuwahi
kufikiri angeshika namba moja kwa ufaulu kitaifa licha ya jitihada zake
za kujituma.
Lakini siku zote Mungu hamtupi mja wake.
Kama jina lake linavyosadifu mwezi mtukufu unaomalizika siku mbili
zijazo, Ramadhani ambaye amehitimu Shule ya Wavulana ya Feza jijini Dar
es Salaam, ameibuka mwanafunzi bora nchini kati ya waliofanya mtihani
huo wa kujiandaa kwa masomo ya elimu ya juu.
“Nilitegemea ningefaulu lakini siyo kwa kiwango hicho… hii ni ‘surprise’ (shtukizo),” alisema Gembe alipohojiwa na Mwananchi baada ya matokeo ya kidato cha sita kutangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa.

“Nawashukuru
wazazi, walimu, ndugu na wanafunzi wenzangu kwa kunipa ushirikiano.
Nilikuwa nafanya sana ibada hivyo haya matokeo ni juhudi binafsi na
majibu ya Mungu,” alisema Ramadhani aliyesoma mchepuo wa fizikia, kemia na baiolojia (PCB).
Historia ya Ramadhani darasani si haba kwani mwaka 2008 alikuwa ni mwanafunzi pekee aliyejiunga na shule ya vipaji maalumu ya Ilboru, Arusha akitokea shule ya Msingi Mombo na alipata daraja la kwanza akiwa na pointi 11 katika matokeo ya kidato cha nne.

“Siku zote kilichonifanya niongeze
juhudi katika masomo yangu ni malengo ya baadaye… mimi nataka kuwa
daktari wa binadamu hivyo sikutaka kulegalega kusoma. Pia, wazazi wangu
pamoja na hali ngumu walijitahidi kunisaidia kimawazo, kirasilimali na
kimaadili…naomba na wazazi wengine wawafanyie hivyo watoto wao,”
alisema.
Nurdin Gembe, ambaye ni mzazi wa Ramadhani, alisema familia imepokea kwa furaha matokeo hayo na kwamba alikuwa akiyategemea kuwa mazuri kutokana historia ya kijana wake katika madarasa ya nyuma.
Nurdin Gembe, ambaye ni mzazi wa Ramadhani, alisema familia imepokea kwa furaha matokeo hayo na kwamba alikuwa akiyategemea kuwa mazuri kutokana historia ya kijana wake katika madarasa ya nyuma.
“Huyu mtoto namlea kawaida japo zamani
alikuwa mtundu sana… ilibidi nimpe mafundisho mengi sana ya kidini bila
kupoteza ratiba ya kusoma shuleni. Nashukuru kuwa alizingatia na amefika
hapo alipofika,” alieleza Gembe ambaye ni bwana shamba kitaaluma.
Kwa upande wake Yonazi Senkondo, aliyeshika nafasi ya tisa kitaifa, alisema matokeo hayo ni majibu ya maombi kwa Mungu na juhudi zake kusoma na ushirika na wanafunzi wenzie.
Kwa upande wake Yonazi Senkondo, aliyeshika nafasi ya tisa kitaifa, alisema matokeo hayo ni majibu ya maombi kwa Mungu na juhudi zake kusoma na ushirika na wanafunzi wenzie.
“Siku
zote nilikuwa naombea niingie 10 bora, najua leo Mungu amejibu maombi
yangu. Nilikuwa nafanya mijadala na wanafunzi wenzangu hasa huyo
aliyeshika namba moja. Sishangai yeye kuwa katika ngazi hiyo.

Note: Only a member of this blog may post a comment.