Monday, July 20, 2015

Anonymous

MBASHA: MIMI NA FLORA NDIYO BASI TENA!

Mwanamuziki wa Injili, Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha enzi za furaha.
Brighton Masalu
Mwisho wa reli? Aliyekuwa mume wa mwanamuziki wa Injili, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha ameapa kwa kulamba kidole, kukichovya kwenye mchanga kisha kukipitisha shingoni kuwa, hana mpango wa kurudiana na mkewe huyo katika maisha yake, Ijumaa Wikienda linakumenyea.

Akizungumza na gazeti hili wikiendi iliyopita, Mbasha aliweka wazi maumivu aliyokuwa akiyapitia wakati akiwa kwenye ndoa na Flora hivyo ameona njia bora ya kujipatia furaha ni kumuacha aishi maisha yake na yeye afanye yake.

Mbasha alikiri kufanya jitihada za ziada akiwatumia ndugu, jamaa na marafiki kumshawishi Flora kurejesha upya penzi lao, lakini amekuwa akiambulia maneno makali na matusi.
“Mimi na Flora basi tena, acha ibaki historia, amenitesa sana kihisia,” alisema Mbasha.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.