MUNGU mkubwa! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia
siha ya mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ ambaye kwa sasa yupo fiti baada ya
kuugua kwa muda mrefu.
Mwaka
jana, mama Diamond aliripotiwa kushambuliwa na maradhi yaliyoashiria
kupooza hadi kufikia hatua ya kwenda kutibiwa India kisha kurudishwa
nchini akiwa bado hajapona vizuri.
Chanzo kilicho karibu na familia ya staa
huyo kilieleza kuwa, ugonjwa huo ambao ulimfanya ashindwe kutembea
vizuri, ulimsumbua kwa kipindi kirefu lakini kwa sasa wanamshukuru
Mungu, mama huyo anaweza kutembea mwenyewe na kuendelea na shughuli zake
za kila siku.
“Wee
ile ilikuwa hatari, ameumwa sana jamani mama Diamond. Hadi hatua hii
ambayo amefikia kwa sasa, kwa kweli tunapaswa kumshukuru sana Mungu,
ameteseka vya kutosha, sasa hivi ukimuona, shavu dodo,” kilisema chanzo
hicho.
Mwanahabari wetu baada ya kupenyezewa
habari hiyo, hivi karibuni alitumiwa picha ya mama Diamond akiwa fiti
akitembea barabarani akifanya shughuli zake za kila siku.
Jitihada
za kumpata mama Diamond azungumzie uzima wake hazikuzaa matunda
kufuatia simu yake ya mkononi kutokuwa hewani lakini Diamond alipatikana
na kusema yeye pamoja na bebi wake, mama kijacho, Zarinah Hassan ‘Zari
The Boss Lady’ wanamshukuru Mungu kwani sasa mama yao yuko vizuri
kiafya.
“Mama
ndiyo faraja yangu siku zote. Kwa kumuona hivi mzima sasa hivi, mimi na
bebi wangu (Zari) tuna amani na tunamshukuru sana Mungu, mama anatembea
na kufanya shughuli zake kama zamani,” alisema Diamond.
Note: Only a member of this blog may post a comment.