Mgeni
rasmi ambae pia ni rais wa Makampuni ya Convivium Africa Investment,
Bw. Alfonso Ippolito akizungumza machache wakati wa uzinduzi wa platform
mpya ya matangazo iliyozinduliwa hapo jana katika hoteli ya serena.
Paisha ni platform ya matangazo ambayo inapatikana kupitia simu za
mkononi yaani smartphone na kupitia tovuti ambapo watumiaji wa simu za
smartphone wanaweza kuipakua kupitia google play and playstore bure
kabisa.
Meneja
bidhaa wa Paisha, Godfrey Fataki akizungumzia jinsi paisha inavyofanya
kazi na faida zake wakati wa uzinduzi wa platform hiyo uliofanyika jana
katika hoteli ya serena
Mgeni rasmi akifungua pazia kuashiria kuwa Paisha imezinduliwa rasmi .
Mtangazaji
wa Redio Clouds Ephraim Kibonde akiwa katika picha ya Pamoja na Balozi
wa Paisha wakati wa uzinduzi wa platform mpya ya matangazo
iliyozinduliwa jana katika ukumbi wa Marquee Serena Hotel.
Mdau
akiwa pembeni ya mfano wa simu ya Iphone ambayo inaonyesha application
ya Paisha.Paisha inapatikana kupitia playstore na google store bure na
endapo utakuwa na application hiyo utaweza kufahamu na kupata huduma
zote zitolewazo nchini huku wateja takribani Milioni 1 wameshajiunga
huku watumiaji wakipata urahisi wa huduma hizo
…Tukipata selfie
Black Ryhino akipata selfie na mabest zake wakati wa uzinduzi huo
Ni mwendo wa selfie tu
Wadau wakifuatilia uzinduzi wa application ya Paisha
Paisha ni platform ambayo inapatika
katika simu za smartphone pamoja na tovuti platform hii ni kwaajili ya
watoa huduma na wauzaji wa bidhaa ambao wanapenda kuwafikia wateja wao
kirahisi,Paisha inapatikana kupitia google play na playstore huku
watumiaji wa paisha wananufaika kufahamu sehemu ambapo wanaweza kupata
huduma mbalimbali kama vile maduka na hata huduma nyingine sehemu ambapo
watuamiaji hao sio wenyeji au wenyeji lakini hawafahamu baadhi ya
bidhaa zinapatikana wapi.
Ukiwa
na application ya paisha katika simu inakusaidi kufahamu kuanzia ramani
alipo mtoa huduma huyo pamoja na mawasiliano yake mfano umeenda tegeta
na umepata pancha na haufahamu sehemu ilipo gereji ukiwa na paisha
kwenye simu yako itakusaidia kufahamu ilipo gereji ambapo itakuonyesha
jina la gereji iliyopo karibu na wewe hapo huku ikikuonyesha na ramani
pamoja na mawasiliano ya gereji hiyo vilevile kwa bidhaa na huduma
nyingine.
Ni
application ambayo inawalete urahisi watumiaji na watangazaji wa bidhaa
hizo kupitia paisha.kufahamu zaidi kuhusu paisha unachotakiwa kufanya
ni tembelea tovuti yao ya www.paisha.co.tz na vilevile unaweza kupakua
application hiyo kupitia playstore na google play sasa
Kuweza kupata faida zaidi.
Picha na Josephat Lukaza wa Lukaza Blog

Note: Only a member of this blog may post a comment.