Wednesday, July 15, 2015

Anonymous

Magufuli Dar, Polisi na uvamizi Stakishari.. Dawa za Kulevya Airport, Rais UKAWA.. Zisikilize stori zote hapa

Uchambuzi wa magazeti redioni leo umekupita? Nimekurekodia stori zote za magazetini zilizosikika @Clouds.Fm zikiwa na baadhi ya stori hizi kubwa. 

Dk. John Magufuli amesema hataogpa mtu yoyote katika utendaji kazi wake kama atachaguliwa na Watanzania kuwa Rais, UKAWA wamesema watamtangaza mgombea Urais ndani ya siku saba. 

Watu wa Haki za binadamu wameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka dhidi ya tukio la Stakishari, Jeshi la Polisi Tanzania limeahidi kutoa shilingi Mil.50 kwa mtu yoyote atakayetoa taarifa za haraka na zenye usahihi kuhusiana na wahusika wa tukio hilo. 

Mtu mmoja amekamatwa Airport Dar akiwa na dawa za kulevya aina ya Heroin akiwa anazisafirisha kwenda nchini Japan.

Kuna stori nyingine kutoka Rwanda ambako Wabunge wamepiga kura kuunga mkono mabadiliko ya Katiba yatakayomruhusu Rais Paul Kagame kugombea Urais wa nchi hiyo kwa awamu ya tatu.
Hapa chini iko sauti ya stori zote zilizosikika leo kupitia @PowerBreakfast.

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.