Sunday, July 12, 2015

Anonymous

KUMEKUCHA CCM BAGAMOYO!

Mathew Yungwe akiongea na wananchi wa Bagamoyo. Kulia ni James Mbulingwe na  mpambe wa mgombea huyo.
Mkazi wa Bagamoyo akitaja moja ya changamoto wanazokutana nazo.Mtangaza nia akisiliza kwa makini.Mtangaza nia mpya wa Chama cha Mapinduzi wa Jimbo la Bagamoyo Mathew Yungwe. akisaliamiana na wazee baada ya kuomba ridhaa ya kuliongoza jimbo hilo.Wakazi wa Bagamoyo wakisikiliza sera za mtangaza nia mpya wa Jimbo hilo, Mathew Yungwe.
KATIKA kuelekea Uchanguzi Mkuu mwaka huu unaotarajia kufanyika Oktoba, vijana wengi wamejitokeza kuwania majimbo mbalimbali na katika Jimbo la Bagamoyo ambalo linashikiliwa na Mbunge Shukuru Kawambwa kwa miaka 10 mfululizo, tayari kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mathew Yungwe amejitokeza kuwania kiti hicho.

Akiomba ridhaa ya kulitumikia jimbo hilo kwa wananchi wa eneo hilo katika Ukumbi wa Macho Kodo iliyopo wilayani humo, Yungwe amesema iwapo atapata nafasi ya kuwa mbunge, vipaumbele vyake ni katika sekta ya afya, uchumi na mawasiliano, sekta ambazo zimekuwa na misukosuko kwa muda mrefu.

“Nitahakikisha kila Kikundi cha Saccos kinatoa asilimia tano ya faidi yao kwa ajili ya wazee, suala la migogoro ya ardhi inapungua na pia nitaweka misingi na kuboresha Soko la Samaki ili vijana wenzangu wapate ajili ya kudumu kwa kuuza bidhaa hiyo ndani ya nje ya Bagamoyo,” alisema na kutambulisha kauli mbiu yake ni ‘Fikiria Tofauti Kwa Maendeleo Endelevu ya Bagamoyo’.
 (Picha na Habari GPL/Deogratius Mongela )

USIPITWE! JIUNGE NASI FACEBOOK

Subscribe to this Blog via Email :

TOA MAONI YAKO HAPA (MATUSI HAYARUHUSIWI)

Note: Only a member of this blog may post a comment.